728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, March 28, 2017

  KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA NA SERIKALI YATEMBELEA WALENGWA WA TASAF KATIKA KIJIJI CHA MLANDA IRINGA VIJIJINI.

   Baadhi ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na  Serikali za Mitaa wakionyeshwa  mabati aliyoyanunua mmoja wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji cha Mlanda ,Iringa Vijijini ,Bi. Konjeta Lyambafu aliyevaa kitambaa kichwani. Kushoto kwake Mwenyekiti wa kamati hiyo Venance Mwamoto akimkabidhi fedha zilizochangwa na wajumbe kuongeza uwezo wa mlengwa huyo kukamilisha mabati ili aezeke nyumba yake iliyoko nyuma yao kwa bati.
   ‘’Ninaishukuru serikali kupitia TASAF kwa kuniwezesha kuboresha maisha kwa kujenga nyumba ya bati na kumudu kuwatunza na kuwasomesha wajukuu zangu wanane ’’ ndivyo mmoja wa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini Bi. Claudia Kanyita mkazi wa kijiji cha Mlanda, wilaya ya Iringa Vijijini anavyoelekea kuwaeleza wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki .
   Mmoja wa walengwa wa TASAF katika kijiji cha Mlanda wilaya ya Iringa Vijijini Claudia Kanyita akiwa na wajukuu zake watatu alioachiwa baada ya watoto wake kufariki, akitoa maelezo kwa kamati ya kudumu ya bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa iliyotembelea kijiji hicho kuona utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na TASAF. Nyumba inayoonekana nyuma yao imejengwa na Mlengwa huyo kwa ruzuku ya TASAF.Wa  kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Ladislaus Mwamanga.
   Wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge wavutiwa na jitihada za mlengwa wa TASAF Bi.Claudia kijijini Mlanda na kumchangia fedha ili aanzishe mradi wa kumwongea kipato, fedha hizo alikabidhiwa na Waziri Kairuki.
   ‘’Mgeni njoo mwenyeji apone ’’ndivyo ilivyo kwa mlengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini wa  kijiji cha Mlanda wilaya ya Iringa vijijini  Konjeta Lyambafu aliyechangiwa fedha na wajumbe wa  kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa ili aweze kuongezea fedha anazozipata kupitia ruzuku inayotolewa na TASAF kuanzisha mradi wa kujiongezea kipata. Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Venance Mwamoto akimkabidhi fedha hizo mlengwa, kulia kwao ni Waziri Angellah Kairuki . Nyumba iliyoko nyuma yao imeezekwa na mlengwa huyo kwa bati alizozinunua kupitia ruzuku kutoka TASAF  na hivyo kuboresha makazi yake.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti na Utumishi wa Umma na Utawala bora, Angellah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na mmoja wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na TASAF katika kijiji cha Mlunda ,Iringa Vijijini, wakati kamati ya kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa ilipotembelea kijiji hicho kukagua namna walengwa wa Mpango huo wanavyonufaika na mpango huo.
   Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge Utawala na Serikali za Mitaa , Venance Mwamamoto, Waziri Kairuki na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kijiji cha Mlanda , wilaya ya Iringa Vijijini wakati kamati hiyo ilipofanya ziara kijijini hapo kuona namna walengwa wa Mpango huo unaotekelezwa na TASAF wanavyonufaika na ruzuku itolewayo kupitia mfumo wa Uhawilishaji fedha.
  Wajumbe wa kamati ya Kudumu ya bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakilakiwa kwa shangwe na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii,TASAF,katika kijiji cha Mlanda wilaya ya Iringa mkoani Iringa kuona namna walengwa hao wanavyonufaika na fedha za Mpango huo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA NA SERIKALI YATEMBELEA WALENGWA WA TASAF KATIKA KIJIJI CHA MLANDA IRINGA VIJIJINI. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top