728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, March 21, 2017

  INOCENT MELECK AJITOKEZA UBUNGE AFRIKA MASHARIKI

   Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Aliyekuwa mgombea ubunge katika jimbo la Vunjo, Inocent Meleck amechukua fomu ya kugombea Ubunge Afrika Mashariki kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi .

  Meleck amechukua fomu hiyo akiongeza Idadi ya Vijana wengi ambao wamejitokeza kuchukua fomu hiyo katika ofisi ndogo ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam .

  Meleck amesema kuwa yeye amechukua fomu hili aweze kupata nafasi ya kuwa mbunge wa Afrika Mashariki kama wanavyofanya vijana wengine wa CCM hili waweze kuwakilisha nchi.

  Aidha alitumia fursa hiyo kumpongeza Mwenyekiti Wa CCM kwa kuweka mfumo ambao umemuwezesha kila mtu kupata fursa ya kugombea hasa kwa vijana .

  Aidha alitoa Rai kwa wana CCM ambao wana lengo na nia nzuri ya kupata nafasi ya kujitokeza kuchukua fomu kwa kufika Lumumba au Zanzibar kuchukua fomu kwani nafasi hiyo inatoa fursa hiyo kwa vijana.

  Inocent Meleck akisalimia na mpiga picha Mwandamizi wa CCM , Bashir Nkoromo
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: INOCENT MELECK AJITOKEZA UBUNGE AFRIKA MASHARIKI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top