728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Sunday, March 26, 2017

  Harmorapa ni nani?

  Hamorapa ni msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye anapendwa kwa mambo mengi, vingi ikiwemo vioja na vichekesho.Na kwa siku za karibuni amekuwa hakosekani kwemye matukio makubwa makubwa ungeweza kudhani yeye ni Mwanahabari,lakini siyo kweli.

  Juzi juzi alionekana akikimbia kwa kuogopa bastola kwenye tukio la Nape pale St Peters.Ungemuuliza yeye kuwa alifikaje pale kwenye tukio na kukaa mbele vile wala asingeweza kukupa majibu.

  Lakini pia alionekana akiwa katikati ya wajumbe wa Kamati ya Huduma za Jamii kule Clouds TV pale walipoenda kutoa pole baada ya ule unaodaiwa uvamizi wa Makonda.

  Hapo napo ungeweza kumuuliza Harmorapa alifuata kitu gani katikati ya Waheshimiwa wabunge,asingeweza kukupa jibu la kieleweka.

  Huyo ndiye Harmorapa ambaye jana amepewa mkataba wa kuwa Balozi wa Kinywaji cha Swala,ili kijitangaze kupitia kwake.

  Asili yake ni mikoa ya kusini mwa Tanzania.Lakini pia kuibuka kwake kwa kasi kubwa kumetokana na yeye kuwa anahangaika kumuiga mwanamuzuki mwenzake aliywmtangulia kwenye fani aitwaye Harmonise,ambaye pia kwao ni kusini.

  Wana ugomvi mkubwa na msanii huyo Harmonise, ambaye ni member Bendi ya WCB inayomilikiwa na Diamond Platnumz.

  Huyo Harmonise anaishi kinyumba na Wolper (mchumba,wabongo kwa uchumba usioisha😂) Mwanafilamu maarufu Wolper.Ameshampeleka mpaka ukweni Mtwara.Kwahiyo utaona kuwa ugomvi ule unawaunganisha wanamuziki kwa upande mmoja pamoja na wasanii wa filamu kwa upande mwingine.
  Hamorapa pia anaye mpenzi wake ambaye humuita 'Wolper'.Jambo hilo linazidi kumkoroga mwenzake Harmonise.

  Aghalabu wawili hao wanatukanana sana Hamorapa na Harmonise. Hamorapa anadaiwa pia kuchukua kipande cha jina na Harmonise yaani "Harmo".

  Harmonise anaamini mwenzake huyo ameiba kipisi cha jina hilo kwa manufaa yake ya kimuziki ili limpaishe.

  Harmorapa anaenda mbali na kudai kuwa yeye sura yake imefanana na ya Harmonise. Mwenzake anapinga sana hilo.Kuna wakati Harmonise alidai kuwa yeye hawezi kufafanana na Harmorapa kwa sura kwakuwa Harmorapa kafanana zaidi na Kima.

  Hata pale ambapo Diamond alionesha nia ya kumchukua Harmorapa ajiunge na WCB,alikataa akiogopa kuwa ugomvi wake na Harmonise ungezidi kuwa mkubwa.Hivyo anajitegemea kimuziki akiwa chini ya meneja wake.

  Juzi Ijumaa EATV waliwaalika wote ili waingie studio na kuzungumzia ugomvi huo.Harmorapa alitangulia kufika.Baadaye alipowasili Harmonise na kulikuta gari la Meneja wa Harmorapa pale kwenye parking akageuza na kuondoka huku akionesha alama ya tusi kwa kutumia kidole.Hayo aliyasema Hamorapa akiwa studio usiku huo.

  Hayo ndiyo mambo ya Wasanii na wanamuziki. Ugomvi huwaletea umaarufu pia.Umri na kabila tuviweke kapuni.

  Ni mimi

  Kasenyenda
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Harmorapa ni nani? Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top