728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, March 30, 2017

  FULL TIME: SERENGETI BOYS 3 vs 0 BURUNDI


  Na Faustine Ruta, Bukoba

  Timu ya Vijana U17 ya Burudi leo kwenye uwanja wa Kaitaba imeanza mchezo wake wa kwanza wa kirafiki kwa kichapo cha bao 3-0 na Timu ya Vijana
  maarufu kwa jina la Serengeti Boys. 


  Bao la kwanza lilifungwa dakika ya 20 na Muhsin Malima Makame bao la pili lilifungwa dakika ya 38 na Nickson Clement Kibabage huku bao la tatu likifungwa kwa mkwaju wa penati na kepteni  Kevin Nashon Naftal dakika ya 72 baada ya beki wa Burundi kujichanganya kwa kuunawa mpira ndani ya boksi.
  Mchezo wa marudiano wa timu hizi utachezwa Jumamosi hapa hapa kwenye uwanja wa Kaitaba, kabla ya Serengeti kupanda ndege kwenda Jijini Dar es Salaam kucheza na U-17 ya Ghana Jumatatu mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mchezo huo utatanguliwa na hafla ya kuagwa kwa kukabidhiwa bendera.
  Kikosi cha Burundi chini ya Miaka 17 kilichoanza dhidi ya Serengeti Boys ya Tanzania. Picha  na habari/ Faustine Ruta.

  Kikosi cha Serengeti Boys kilichoanza leo kwenye mchezo wa kirafiki kwenye Uwanja wa Kaitaba
  Viongozi mbalimbali walikuwepo


  Mgeni rasmi akisalimiana na Wachezaji wa Serengeti Boys

  Mgeni Rasmi na viongozi wengine wakisalimiana na Viongozi na wachezaji wa akiba wa Burundi

  Nyimbo za mataifa yote mawili ziliimbwa kabla ya mechi kuanza

  Taswira kabla ya mtanange

  Viongozi wa Timu ya Serengeti Boys

  Serengeti Boys wakipasha kabla ya Mtanange

  Picha ya pamoja  Kipindi cha pili kilimalizika Serengeti Boys wakiwa mbele ya bao 2-0 dhidi ya Timu ya Burundi.
  Picha  na habari/ Faustine Ruta.Wanaangalia Mubashara  bila Kiingilio!!!

  Mchezaji wa Serengeti Boys Yohana Oscar Mkomola wa Serengeti akiendesha mpira kipindi cha pili
  Oscar Mkomola(katikati) wa Timu ya Serengeti akiwekwa kati
  Kim na Bakary Shime wakiteta huku mtanange ukionekana kuwa mtelezo kwao kipindi cha pili katika mchezo wa karafiki leo kwenye Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba. Kocha Bakar Shime ataiongoza tena Serengeti Boys siku ya Jumamosi kwenye mchezo wa pili.


  Kipa hakuona kitu!

  Nahodha wa Serengeti Boys  Kevin Nashon Naftali dakika ya 72 ndiye aliyewafungia bao hilo baada ya beki wa Burundi kujichanganya kwa kuunawa mpira ndani ya boksi.

  Mchezaji wa Serengeti Boys (kushoto) akipeta kwa bao lao la tatu

  Bao tatu 3-0

  Serengeti wakifurahia moja ya bao la mkwaju wa penati


  Shangwe! 3-0

  Chupuchupu afunge bao lingine!

  Assad Ally Juma wa Serengeti Boys(kushoto) akiufukuzia mpira

  Clement Kibabane akimiliki mpira kipindi cha pili mwishoni

  Kibabane tena na mpira

  Mchezaji wa Serengeti Boys (kulia) Ibrahim Abdallah Ally akimnyatia mchezaji wa Burundi

  Burundi wakiwa hoi baada ya kuzidiwa ujanja

  Dakika 90 zilikamilika
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: FULL TIME: SERENGETI BOYS 3 vs 0 BURUNDI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top