728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Saturday, March 18, 2017

  DIAMOND AULA UBALOZI WA BIDHAA ZA GSM

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

  Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul (Diamond Platnum) amekuwa Balozi wa Bidhaa za GSM na kuwataka watanzania wanunue bidhaa hizo kuacha kutumia gharama kwa kufuata nje ya nchi.

  Akizungumza leo na waandishi wa habari, Diamond amesema kuwa licha ya kuwa balozi katika bidhaa za GSM ameweza yeye kununua kutokana vitu mbalimbali katika maduka hayo.

  Amesema kuwa GSM walikuwa na uwezo wa kutafuta wasanii wa nje ya nchi lakini wakaona kuna umuhimu wa kuwatumia wasaani wa ndania kama mabalozi katika bidhaa zao. 
   
  "Hivyo katika hilo na kuchangia maendeleo kwa wasanii wetu wa hapa nyumbani,wanaojituma na kuonesha mafanikio yao makubwa kwa kile wanachokifanya,sisi kama GSM tumeamua kutimia msanii Diamond Plutnum kuwa Balozi wa bidhaa zetu" alisema

  Aidha amesema kuwa ubalozi huo utafanya kutangaza muziki wake kwa mashabiki wa ndani na wan je ya nch. Diamond amesema kuwa balozi hakuadhiri ubalozi mwingine kutokana kuwa kinachotangazwa ni bidhaa ambazo haziingiliani. 

   Msanii wa Bongo Fleva,  Nasibu Abdul (Diamond Platnum) akizungumza na waandishi habari baada ya kukabidhiwa ubalozi wa bidhaa za GSM leo jiiini Dar es Salaam.
   Afisa Masoko wa GSM, Lauma Mohammed  akizungumza na waandishi wa habari juu ya Diamond kuwa Balozi wa Bidhaa za GSM leo jijini Dar es Salaam.
   Waandishi wa habari wakimsikilizwa Msanii wa Bongo Fleva,  Nasibu Abdul (Diamond Platnum)  hawapo pichani leo jijini Dar es Salaam. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: DIAMOND AULA UBALOZI WA BIDHAA ZA GSM Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top