728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, March 8, 2017

  CDA YAKANUSHA UUZAJI WA VIWANJA MKONZE

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

  Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) imekanusha juu ya uvumi unaosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu uuzaji wa viwanja katika eneo ka Mkonze lililopo mkoani Dodoma.

  Tamko hilo limetolewa hivi karibuni mkoani Dodoma na Kaimu Meneja Uhusiano wa CDA, Angela Msimbira kutokana na kusambaa kwa ujumbe huo katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

  Bi. Angela amesema taarifa hizo ambazo hazieleweki zimekuwa zikidai kuwa viwanja hivyo ni halali na ukinunua unapewa hati na CDA ambayo ndiyo imepewa dhamana ya ugawaji wa viwanja mkoani humo.

  “Mamlaka yetu inapenda kuutarifu Umma kuwa taarifa hizo si za kweli hivyo wananchi wanatakiwa kuzipuuza na kuendelea kufata utaratibu kwani mamlaka hiyo ina utaratibu uliopangwa wa namna ya kupata viwanja vilivyo halali,”alisema Bi. Angela.

  Amefafanua kuwa Mamlaka hiyo inapotaka kuuza viwanja hutumia utaratibu wa kutangaza kwenye vyombo vya habari, mitandao ya kijamii pamoja na kutoa matangazo kwa umma kwa njia ya vipaza sauti.

  Aidha, Bi. Angela ametumia fursa hiyo kuendelea kuwakumbusha wananchi kufuata taratibu za upatikanaji wa viwanja.

  Kwa mujibu wa kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Jinai Mitandaoni ya mwaka 2015, ni kosa kwa mtu yoyote kutangaza, kuchapisha au kueneza habari za uongo au uzushi katika mitandao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: CDA YAKANUSHA UUZAJI WA VIWANJA MKONZE Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top