728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, March 20, 2017

  BASATA KUTOA TUZO KWA WANAFUNZI WALIOFANYA VIZURI KATIKA MASOMO YA SANAA

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) linataraji kuwazawadia wanafunzi Saba waliofanya vizuri katika sanaa za maonyesho na uchoraji katika shule tano za sekondari nchini.

  Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Masoko wa Basata, Vivian Shaluwa amesema kuwa wameamua kutoa zaidi tuzo ili kuongeza hamasa katika masomo ya Sanaa katika shule za Sekondari.

  “Tuzo hizi zitakuwa nyenzo kwa ajili ya kujenga hamasa, ari, ubunifu na juhudi katika kuleta maendeleo kupitia masomo ya sanaa. Katika program hii wanafunzi kutoka shule 5 za sekondari zitakazohusika katika kupewa tuzo hizo, shule hizi ni Loyola, Azania za Dar es Salaam, Bukoba ya Mkoa wa Kagera, Darajani toka Mkoa wa Kilimanjaro na Arusha Sekondari toka mkoa wa Arusha.Amesema Shaluwa.

  Amesema ni matarajio ya BASATA kuwa utoaji wa tuzo hizi utachochea wanafunzi wengi kusoma masomo ya sanaa, kuongeza ubunifu katika kazi za Sanaa na kuwasaidia katika kuongeza ufaulu wao darasani hasa ikizingatiwa Sanaa ni nyenzo katika kumuandaa mtoto kielimu na kimaadili.

  Mkurugenzi wa Masoko wa Basata, Vivian Shaluwa Akizungumza na Waandishi wa Habri mapema leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Afisa Habari mkuu , Agnes Kimwanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: BASATA KUTOA TUZO KWA WANAFUNZI WALIOFANYA VIZURI KATIKA MASOMO YA SANAA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top