728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, February 27, 2017

  corner bar yafungwa kwa kukiuka taratibu na maadili

  Baada ya malalamiko kuzidi kutokana na kuwapo biashara zisizo rasmi katika baa maarufu ya Corner Bar a.k.a Club Ambiance, iliopo maeneo ya Afrika sana (Sinza) sasa baa hiyo imeamriwa kufungwa.
  Akiwa katika ziara ya kawaida mwishoni mwa wiki (Jumamosi) Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amemuagiza Ofisa Biashara wa Kinondoni, Mohamed Nyasama kuifunga baa hiyo.
  “Hatuwezi kuvumilia vitendo hivi vikaendelea kufanyika huku tukiwa kimya…natoa agizo kesho.nendeni kaifungieni hiyo baa kwa kuwa inakiuka maadili,”amesema Hapi.Hata hivyo Nyasama amesema walishaitoza baa hiyo faini ya Sh 300,000 kwa kosa hilo.
  “Mkuu hii baa ni sugu, nimewahi hata kuipiga faini na bado imeendelea na utaratibu huo huo wa kuruhusu kina dada kujiuza.Kwa amri yako mkuu naanza taratibu za kuifungia leo, hadi kufikia kesho itakuwa tayari,” amesema.

  Source: Mwananchi
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: corner bar yafungwa kwa kukiuka taratibu na maadili Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top