728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, January 12, 2017

  MAJ.GEN.GAUDENCE; UJANGILI KWA SASA UMEPUNGUA NCHINI

  Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi akizungumza katika mkutano huo.luv1
  Picha ya pamoja
  ……………………………………………………………………………………….
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii amesema kwa kiasi kikubwa cha  ujangili umepungua nchini na kwamba meno ya tembo yanayokamatwa kwa sasa ni masalia ya zamani.
  Aliongeza kuwa kinachohitajika kwa sasa ni kuendelea kufuatilia kuwa nani anaua,nani anatoa porini na nani mnunuzi ili wote wakamatwe na hatua kali zichukuliwe dhidi yao ili iwe fundisho.
  Katika hatua nyingine Katibu Mkuu amepongeza hatua ya nchi ya China kuua soko la manunuzi ya meno ya tembo ,jambo ambalo alisema litafanikisha zaidi ujangili kupungua.
  Alisema si tu china bali kuna nchi nyingine ambazo zinajihusisha na manunuzi hayo zinatakiwa kuunga mkono usitishwaji huo ili uuaji wa wanyama hai uishe kabisa.
  Aidha, Milanzi amesema serikali imeweka mpango mkakati mpya wa kuhakikisha ujangili unaendelea kudhibitiwa kwa hali ya juu.
  Pia amewataka watumishi wa Mamlaka ya Usimamamizi wa Wanyamapori (TAWA) wametakiwa kutojifungia maofisini na badala yake kuingia kufanya kazi katika maeneo yao kazi yaani ‘field’ hapo ndipo mafanikio yatatokea.
  Hayo aliyasema jana wakati akizungumza kwenye mkutano ulioandaliwa na Mamlaka ya Usimamizi wa wa Wanyamapori Nchini (TAWA) walipokutana na  wahifadhi wakuu kwa lengo la kuweka mkakati wa udhibiti wa ujangili.
  Alisema kila mfanyakazi na kila mtu aliyepo katika mamlaka hiyo anatakiwa kujitafakari yeye mwenyewe kwa utendaji wake.
  Alisema hakuna sababu ya kushindwa kukabiliana na ujangili na huku akiwataka kusiwe na sababu kukosa hiki wala kile kinachohitajika ni mambo ya maendeleo pekee.
  Hata hivyo alisema kuna watumishi ambao wanajihusisha na ujangili lakini hafikirii kama wote ni watu wabaya bali wenye kasoro hiyo wapo hivyo watumishi wema wasikubali wakawavurugwa na wengine.
  Naye Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali (DPP) Biswalo Mganga amesema watu ya 200 wamekamatwa katika kipindi cha mwaka jana kutokana makosa ya kukutwa na nyara mbali mbali za Serikali.
  Pia zaidi ya milioni 800-900 zilipatikana kutokana na faini za watu wanaokutwa na nyara za serikali sambamba na walioshindwa kulipa faini kufungwa miaka 20-25.
  Alisema kati ya watuhumiwa hao endapo wote wangefanikiwa kutoa faini na kutofungwa kiasi cha shilingi bil 164 zingekusanywa na kwamba hiyo inaonesha ni jinsi gani udhibiti unaendelea kwa kasi .
  Biswalo alisema kutokana na takwimu hizo kwa mwaka huu hawatategemea kutokea tena kwani idadi hiyo ilikuwa kubwa na inatisha kwa taifa.Alisema kila mmoja anajukumu la kulinda maliasili za serikali ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za wahalifu hao ili ziweze kushughulikiwa haraka na kufunguliwa mashitaka.
  Kaimu Mkurugenzi wa TAWA,  Martini Loibooki alisema vita ya ujangili ni kubwa hivyo inahitaji kuongeza nguvu ili kuwazuia waharifu wenye ushawishi.Alisema wanafahamu kuna watumishi wengine wanahusika katika ujangili hivyo katika mwaka huu wanatakiwa kuacha mara moja.
  ‘’Hadi sasa kuna watumishi wanne ambao wanachunguzwa kujihusisha na hilo na endapo wakibainika hatua mbalimbali za kisheria zitachukuliwa,’’alisema.Naibu wa Mkuu wa Jeshi la Polisi Abdulrahman Kaniki alisema ni jukumu kwa jeshi la Polisi kulinda rasilimali za taifa ili vizazi vijavyo viweze kuona kuliko kuadithiwa.
  Alisema ni muhimu kuona wanajipangaje hasa katika kuwa na mahusiano mazuri kwa sekta mtambuka katika kuhakikisha ujangili unakwisha.lisema ni vyema kuwakamata watuhumiwa kuwepo na ushahidi wenye taarifa sahihi ,ili hatua dhidi yao ziweze kuchukuliwa bilakuonewa.
  Naye mhifadhi mkuu wa Pori la Akiba la Selous Henock Msocha alisema mafunzo haya ni sahihi kwa kuwa wanakumbushana mambo mengi na kuwafanya wajirekebishe kwa kile walichokosea awali.
  Mwenyekiti wa bodi ya TAWA meja Mstaafu Hamis Semfuko,alisema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na maeneo ya kuwaweka watuhumiwa.Pia alisema rushwa ni malalamiko ya wengi na miongoni mwa watumishi wanajihusisha na uhalifu.
  Alisema ufanisi unahitajika na kujibidiisha ili kuongeza kasi ya utendaji kazi kwa TAWA.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MAJ.GEN.GAUDENCE; UJANGILI KWA SASA UMEPUNGUA NCHINI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top