728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, December 1, 2016

  KAMPUNI YA UWEKEZAJI YA TAIFA (NICOL) KUIBUKA UPYA BAADA YA KUINGIA HASARA YA BILLIONI 10

  Mwenyekiti wa kampuni ya Uwekezaji wa Taifa (NICOl) Bw. Gideon Kaunda kulia akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es salaam mara baada ya kupata uongozi mpya wa kampuni hiyo ulioteuliwa rasmi hivi karibuni na bodi ya NICOL kushoto ni Mtendaji Mkuu Bw. Adam Wamunza.


  Na Amina Kibwana,Globu ya Jamii

  Kampuni ya Uwekezaji ya Taifa (NICOL) inatarajia kurudi upya mara baada ya kuingia hasara ya sh. Billion 10 pamoja na kukabiliana na kesi Mbalimbali ikiwemo  kupinga maamuzi ya wanahisa kuchagua uongozi pamoja na maamuzi ya kusitishwa kwa mkutano mkuu uliolenga kuzungumzia maswala ya mahesabu na muelekeo wa Kampuni.

  Akizungumza na waandishi wa Habari  Mwenyekiti wa NICOL Dk. Gideon Kaunda amesema kuwa kesi ya mwisho ya 41 iliamuliwa  mahakamani mara baada ya Mlalamika  makamu mwenyekiti wa TPSF Salum Shamte kutokuhudhuria mahakamani na hoja hizo zilikataliwa na Mahakama kuamua kuwa mkutano huo ulikuwa wa halali na ambapo mnamo Novemba 26 mkutano huo uliendelea.

  “Mkutano ulikwenda vizuri ambapo zaidi ya watu 300 kutoka mikoa mbalimbali walihudhuria pamoja na mashirika mbalimbali ya umma ambayo yalikuwa yamewekeza  wakiwemo PSPF, walifanikiwa kuhudhuria”. Alisema Kaunda 

  Aidha alisema kuwa Kampuni hiyo iliingia hasara kutokana na  uongozi uliopita kuwa na malimbikizo ya sh. Billion 10 kutokana na mahesabu yaliyofanywa, ambayo taarifa ilionesha kuwa kampuni ilikuwa inapata faida kwa wakati huo  sio sahihi,pamoja na kutokufuatwa kwa sheria na utovu wa nidhamu.

  Kwa upande wake Mtendaji  Mkuu wa NICOL  Adam Wanuza amesema kuwa kuwa pamoja na hasara hiyo,ukiwemo uwekezaji mbovu umechangia kutokana na makampuni mbalimbali kuchukua mkopo katika Kampuni ya Nicol.

  Naye Naibu Waziri Mstaafu katika sekta ya Uchukuzi ambaye pia ni Mtaalamu katika Masuala ya Biashara Dk. Athumani Mfutakamba amesema kuwa kufanikiwa kwa Mkutano huu ni ishara tosha ya kuzaliwa upya kwa NICOL katika jitihada za Kampuni ya uwekezaji ya kizalendo na jitihada hizi lazima ziungwe mkono na wazalendo wote wanaotaka maendeleo ya uchumi wa Taifa la Tanzania katika fursa mbalimbali.

  Kampuni ya Nicol itarudi Rasmi kupitia uongozi mpya sambamba na kuanza kutoa elimu Maalumu kwa wawekezaji katika soko la Hisa mnamo mwanzoni mwa mwaka 2017.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: KAMPUNI YA UWEKEZAJI YA TAIFA (NICOL) KUIBUKA UPYA BAADA YA KUINGIA HASARA YA BILLIONI 10 Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top