728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, November 14, 2016

  WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR AZUNGUMZA NA WANDISHI WA HABARI KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA KISUKARI DUNIANI

  Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Mnazi mmoja katika kilele cha maadhimisho ya siku ya kisukari duniania.

  Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

  …………………………………………………..

  Na Ramadhani Ali-Maelezo

  Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo amesema hadi sasa hakuna dawa yoyote duniani iliyothibitishwa kutibu ugonjwa wa kisukari na amewashauri watu waliopata maradhi hayo wawe karibu na madaktari kupata miongozo sahihi itakayowasaidia kuimarisha afya zao

  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mnazi mmoja katika kilele cha kuadhimisha siku ya kisukari duniani, Waziri Mahmoud amesema ugonjwa huo ni hatari na ni miongoni mwa magonjwa makuu matano yanayoongoza kwa kuuwa watu wengi Zanzibar.

  Amesema kwa kawaida ugonjwa wa kisukari huchelewa kujitokeza dalili zake na zinapojitokeza tatizo tayari linakuwa kubwa hivyo amewataka wananchi kujenga utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara ili kama kuna dalili zozote wapate ushauri wa kitaalamu na hatimae kuepusha athari zaidi.

  Ameongeza kuwa maradhi ya kisukari yanaweza kukingwa kwa asilimia 80 iwapo wananchi watajiepusha na vihatarishi vinavyopelekea kupata ugonjwa huo.

  Ametaja changamoto inayojitokeza katika maradhi hayo hivi sasa ni kuwa watoto wadogo nao wamekuwa wakipata ugonjwa huo kwa kasi na kwa mujibu wa takwimu wastani wa watoto 230 wamesajiliwa katika hospitali ya Mnazi mmoja na Abdalla Mzee na zaidi ya watoto 20 wamepoteza maisha kati ya mwaka 2010 hadi 2015.

  Amesema tatizo jengine lililojitokeza kwa mujibu wa vipimo vilivyo fanywa katika Wizara nane za Serikali imegundulika kuwa idadi kubwa ya wafanyakazi wanakabiliwa na tatizo la maradhi ya kisukari.

  Amewataka wananchi kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi na kuwa na utaratibu mzuri wa vyakula kwani ni moja kati ya tiba nzuri ya maradhi ya kisukari.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR AZUNGUMZA NA WANDISHI WA HABARI KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA KISUKARI DUNIANI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top