728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, November 11, 2016

  WAZIRI UMMY MGENI RASMI KONGAMANO LA AFYA TANZANIA

  Na Ally Daud-MAELEZO

  AZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano la tatu la kitaifa la Afya litakalofanyika Novemba 14 mwaka huu Jijini Dar es salaam. 

  Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Rais wa Kamati ya maandalizi ya mkutano huo, Dkt. Omary Chillo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es salaam wenye lengo la kujadili maendeleo ya sekta afya nchini. 

  Aidha Dkt. Chillo alisema kuwa kongamano hilo litajadili jitihada ilizofikia Tanzania katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya kimkakati ya maisha yenye afya njema (SDG-3) yaliyokusudiwa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya wachapakazi. 

  Dkt. Chillo aliongeza kuwa kongamano hilo pia linatarajia kujadili mikakati ya kuboresha sheria ya usalama na afya makazini, kanuni na ufanyaji kazi nchini kwa ajili ya maendeleo ya wafanyakazi na usalama wao. 

  Kwa mujibu wa Dkt. Chillo alisema kuwa kongamano hilo pia linatarajiwa kufanyika kuwakutanisha wataalam wa sekta ya afya 700 na kuratibiwa na taasisi tano zikiwemo MoHCDGEC, TMHS,APHFTA,CSSC na BAKWATA. 

  Mkutano huo ambao utakutanisha taasisi 53 za afya, zinatarajia pia kushiriki katika maonesho ya bidhaa zinafanyika kwa ushirikiano wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto pamoja na TAMISEMI tangu kuanza kwake 2014.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: WAZIRI UMMY MGENI RASMI KONGAMANO LA AFYA TANZANIA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top