728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, November 9, 2016

  WATUMISHI WA UMMA WAZINGATIE UMUHIMU WA MAADILI YA KAZI ILI KUKUZA UCHUMI.

  Na Amina kibwana,Globu ya jamii  

  Tume ya Utumishi wa Umma imewataka wafanyakazi wa Umma kuzingatia umuhimu wa maadili wanapotekeleza kazi ili kukuza uchumi na kutoa huduma bora kwa wananchi. 

  Akizungumza na waandishi wa habari Katibu Msaidizi wa tume hiyo Peleleja Masesa amesema kuwa utendaji wa kazi katika  utumishi wa Umma  huongozwa na maadili ya kazi ambayo yameainishwa na serikali, ambapo viongozi na watumishi wote wa umma hawana budi kufanya kazi kwa kufuata Sheria,kanuni,Taratibu na Miongozo mbalimbali ambayo ipo.

  Masesa amesema kuwa zipo kanuni mbalimbali za maadili kama kutoa huduma bora, kufanya kazi kwa Bidii, Utii wa Sheria,Kufanya kazi kwa uadilifu,kuheshimu sheria na kutoa huduma bila upendeleo mabazo zinawaongoza watumishi wa Umma wanapokuwa wanatimiza majukumu yao ya kazi ili waweze kutatua matatizo ya wananchi.

  Pia Masesa ameongeza kuwa Matarajio ya wananchi kwa serikali ni kupata huduma bora toka kwa Viongozi na watumishi wa Umma waliopewa dhamana ya kuwa katika ofisi za Umma kwa lengo la kuleta matumaini katika kutatua matatizo yao.

  “Ili kukidhi matarajio ya watanzania na kumudu jukumu la kuwa nguzo muhimu kwa maendeleo na ustawi wa Taifa letu watumishi wa Umma hatuna budi kuzingatia maadili, Kutanguliza maslahi ya Umma na kuzingatia sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa wakati wa kutoa huduma.”

  Katika kuhakikisha kuwa maadili katika Utumishi wa Umma yanazingatiwa,  Serikali imetoa wajibu kwa Mamlaka za ajira na Nidhamu za watumishi wa Umma na Wajibu wa Tume ya Utumishi wa Umma katika usimamamizi wa rasilimali watu ili ziweze kuwachukulia hatua za Kinidhamu Watumishi wa Umma ambao wanakiuka Maadili pamoja na kuhakikisha kuwa waajiri katika utumishi wa Umma wanasimamia rasilimari watu kwa kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo.

  Tume ya Utumishi wa Umma inawataka waajiri,Mamlaka za ajira na Nidhamu na watumishi wote wa Umma kuzingatia kanuni za Maadili wakati wote wa utekelezaji wa Majukumu ili kukuza Uchumi, kutoa Huduma bora na kulinda amani na utulivu wa nchi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: WATUMISHI WA UMMA WAZINGATIE UMUHIMU WA MAADILI YA KAZI ILI KUKUZA UCHUMI. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top