728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, November 24, 2016

  WASAFI WAOMBA MAMBO MATANO KWA NAPE.  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye  akizungumza na  Mmiliki wa Wasafi Classic Msanii Naseeb Abdul (Diamond Platinumz) wakati alipotembelea Studio za Wasafi Classic kujionea utendaji kazi wa studio hiyo Novemba 23,2016.
  wasf2
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na Mmiliki wa Wasafi Classic Msanii Naseeb Abdul (Diamond Platinumz) na wasanii harmonize na Rich Mavoko.
  …………………………………………………….

  Kundi la Muziki wa kizazi kipya(Bongo Flavour) Wasafi limemuomba Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye   kusaidia wasanii wa muziki huo kujivunia kazi yao kwa kupata maslahi ya kazi hiyo kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

  Akizungumza wakati Waziri huyo alipotembelea Studio za Wasafi na kujionea utendaji kazi wa studio hiyo, Mmiliki wa studio hizo Naseeb Abdul (Diamond Platinumz) amesema, kumekuwa na changamoto nyingi katika tasnia ya muziki hasa wizi wa kazi zao ambazo zimekuwa zikirudufiwa na kuuzwa kiholela ndani na nje ya nchi bila wao kufaidika na uuzwaji wa kazi hizo.

  Changamoto nyingine alizozitaja  msanii Diamond ni pamoja na kupunjwa mapato yatokanayo na Miito ya Simu (Caller tunes) , kukosekana kwa ukumbi wa kisasa kwa ajj ili ya kufanyia maonesho makubwa ya muziki nchini, kuongezeka kwa uwiano wa nyimbo za kitanzania zinazopigwa redioni dhidi ya nyimbo za kigeni hasa kutoka Afrika ya Magharibi.

  Aidha wamemuomba Waziri Nape Moses Nnauye kuwasaidia kupata Elimu juu ya ulipaji kodi ili tasnia ya Muziki nayo iweze kuwa kati ya tasnia zenye mchango mkubwa kwa pato la taifa kwa maendeleo ya wasanii na taifa kwa ujumla.

  Kwa upande wake Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye  amehaidi kuzifanyia kazi changamoto hizo na kuifanya tasnia ya muziki kuwa ajira kubwa kwa vijana wengi kwa kuongeza vipato vyao na pato la taifa kwa ujumla.

  Wasafi Classic ni kundi la Muziki wa kizazi kipya(Bongo Flavour) Tanzania linalomilikiwa na Msanii Naseeb Abdul (Diamond Platinumz) na mpaka sasa lina wasanii wapatao 16 na linaongozwa na mameneja Babu Tale, Said Fella na Sallam SK.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: WASAFI WAOMBA MAMBO MATANO KWA NAPE. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top