728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, November 17, 2016

  WALEMAVU WANAKOSA FURSA ZA KUPATA AJIRA KUTOKANA NA KATOKUAMINIWA- WAZIRI POSSI

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
  NAIBU Waziri,Ofisi Waziri Mkuu,Sera,Vijana na Walemavu,Abdalla Possi amesema kuwa fursa nyingi za ajira kwa walemavu zinakosekana kwani wengi wao wanaona kama hawawezi kufanya kazi kwa ufasaha kitu kinachoplekeka kuwanyima fursa za kuonyesha uwezo wao.

  Akizungumza hayo katika Semina iliyoandaliwa na Association of Tanzania Employment (ATE) wakishirikiana na Shirika la kazi Duniani (ILO), Possi amesema kuwa vijana wanatafuta ajira ila wanashindwa kupata kutokana na fursa kuwa chache ila kutokana na mradi huu utasaidia sana kuweza kuwawezesha vijana kujiajiri na hata kuwa watendaji wazuri wa kazi katika ofisi wanazofanyia kazi.

  Possi amesema kuwa tatizo la jira ni kubwa sana na kundi kubwa wanaloathirika ni walemavu pale wanaposhindwa kuaminiwa na wenye makampuni yao au ofisi zao kwa kuona kwua hawataweza kufanya kazi kwa uweledi. ''wengi wao wanaona kama walemavu hawawezi kufanya kazi nzuri kwahiyo wanashindwa kuwapa fursa za ajira, kwani ni wangapi wanakuwa na elimu nzuri lakini wanashindwa kupata ajira zaidi wanakuwa hawapewi fursa''.

  Serikali tayari ina nia ya kukutana na waajiri na makampuni ya Mafunzo pia kuna Mfumo wa kitaifa unaotarajiwa kupitishwa, utakaokuwa na mwongozo wa kazi zetu zote katika mafunzo nchini na pia amewataka waajiri kuchangia mipango ya mafunzo mahali pa kazi.

  Mkurugenzi wa Association of Tanzania Employment (ATE), Aggrey Mlinuka amesema kuwa hii ni fursa kwa vijana kuwa wabunifu zaidi katika kazi zao na pia hii inakuwa msaada mkubwa kwa makampuni kuweza kuwalipia wafanyakazi wao ili kuja kupata uelewa zaidi wa nini wanatakiwa kufanya katika kushughuli zao za kikazi na sio kwa wafanyakazi tu hata vijana wengine waliomaliza vyuo wanaweza kujitokeza kupata elimu hiyo.

  Kwa kuzingatia changamoto za utandawazi ambayo inaruhusu usafirishaji huru wa kazi kati ya nchi, tunapaswa kuweka juhudi za makusudi na za pamoja ili kufanya watu wetu wengi wawe katika soko la ajira. Tunahitaji kuwawezesha wafanyakazi wetu kwa tija na ushindani ili kuchukua faida ya fursa za biashara ambayo hupatikana katika Afrika Mashariki Soko la Pamoja la na nje ya nchi.

  Ofisa Mkuu wa Shirika la Kazi la Duniani (ILO) nchini, Jealous Chirove amesema kuwa mabadilko ya utandawazi yanachochea mataifa mbalimbali kufanya kazi kwenye mataifa mengine yametufanya sisi kama ILO nchini Tanzania kujizatiti katika kutoa elimu kwa vijana wetu ili wawe na uelewa mkubwa sana katika soko la ajira duniani.

  Chirove amesema kwa ufupi mkakati huu unaweza kusaidia kuboresha matokeo ya ajira kwa wahitimu vijana wakati huo huo makampuni kupata faida ya kuajiri vijana waliokuwa tayari wameiva katika kujua umuhimu wa kazi na pia ripoti ya mwaka 2014 juu ya soko la ajira kwa wanawake vijana na wanaume nchini inaonyesha kwamba kuna uwezekano wa kuwa ongezeko kubwa la ajira na kiwango cha elimu.
  Naibu Waziri,Ofisi Waziri Mkuu,Sera,Vijana na Walemavu,Abdalla Possi akizungumza na waandishi wa habari juu ya malengo ya serikali ya kukutana na waajiri na makampuni yanayotoa elimu kwa vijana kuhusiana na fursa za ajira na pia namna walemavu wanavyoshindwa kupata ajira kutokana na kutokuwwepo kwa imani nao.
  Mkurugenzi wa Association of Tanzania Employment (ATE), Aggrey Mlinuka akitolea ufafanuzi jinsi ya mradi huo utakavyowasaida vijana hususani walioamliza vyuo na hata wale wanaofanya kazi kuweza kupata elimu itakayowawezesha kufanya kazi kwa uweledi.
  Ofisa Mkuu wa Shirika la Kazi la Duniani (ILO) nchini, Jealous Chirove akielezea namna wanavyopambana katika kuhakikisha vijana wa kitanzania wanakuwa wengi kwenye soko la ajira na kuongeza wigo wa upatikanaji wa ajira.
  Naibu Waziri,Ofisi Waziri Mkuu,Sera,Vijana na Walemavu,Abdalla Possi akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Association of Tanzania Employment (ATE), Aggrey Mlinuka wakati wa uzinduzi wa semina hiyo leo Jijini Dar es salaam.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: WALEMAVU WANAKOSA FURSA ZA KUPATA AJIRA KUTOKANA NA KATOKUAMINIWA- WAZIRI POSSI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top