728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, November 2, 2016

  WAANDISHI WATUMIE KALAMU ZAO KUELIMISHA UMMA JUU YA USALAMA BARABARANI

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
  MWANDAMIZI wa masuala ya usalama barabarani , Lawrence Kilimwiko amewataka waandishi wa habari  kutumia kalamu zao kuelimisha umma juu ya usalama bora na namna ya kukabiliana nazo.

  Akitolea ufafanuzi juu ya masuala ya usalama barabarani, Kilimwiko amesema kuwa waandishi wengi wa habari wanaripoti habari za ajali kama matukio na kushindwa kufuatilia hasa baada ya kumaliza kuandika hawafanyi ufuatiliaji wa majeruhi.

  Kilimwiko amesema kwa ajali za barabarani zimekuwa janga la afya hasa baada ya takribani watu milioni 50 wanaathirika na ajali hizo na wengine kupoteza maisha  na kundi kubwa linaloathirika ni vijana na inakadiriwa kufika mwaka 2030 ajali za barabarani zitachukua namba 5 katika janga la vifo duniani.

  Kutokana na ajali hizo, zimesababisha kupeleka mzigo mkubwa kwa sekta ya afya na kupelekea kuongeza gharama za serikali na kuchangia umasikini kutokana na nguvumali ya taifa kuangamiakwa ajali za barabarani.

  Uchunguzi uliofanyika kupitia Shirika la Afya Duniani(WHO) kupitai usalam barabarani  wamegundua kuwa asilimia 95 za  ajali zinatokana na matumizi mabya ya barabara na kuhamasisha waandishi wa habari kusaidia na kuchochea mabadiliko ya sera za sheria za Usalama barabarani.

  Kilimwiko amesema nchi kama Afrika Kusini ina sheria ambayo dereva yoyote haruhusiwi kutumia simu wakati anaendesha chombo cha moto na atakapokamatwa basi atapigwa faini na hili linatakiwa kufanyika hata nchini kwetu na hilo litasaidia kupunguza ajali.
   Mwandamizi wa masuala ya Usalama Barabarani, Lawrence Kilimwiko akizungumza na waandishi wa habari juu ya masuala ya Usalama barabarani na jinsi ya kuelimisha jamii kuhusiana na sera za usalama bwa barabara katika semina elekezi kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA).
  Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa makini kumsikiliza mwandamizi wa masuala ya usalama barabarani Lawrence Kilimwiko.Picha na Zainab Nyamka,

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: WAANDISHI WATUMIE KALAMU ZAO KUELIMISHA UMMA JUU YA USALAMA BARABARANI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top