728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, November 24, 2016

  Ukosefu wa Ajira ni Matokeo sio Janga barani Afrika-Profesa Ole Gabriel

  Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii

  Katibu mkuu wa Wizara ya habari  Sanaa na michezo Profesa Elisante Ole Gabriel amesema kuwa tatizo la ukosefu  wa ajira Afrika ni matokeo na sio tatizo kama watu wanavyosema ama dhania.

  Profesa Gabriel amesema hayo katika Mdahalo wa wanazuoni  kutoka Afrika Mashariki uliofanyika katika ukumbi wa mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.

  "Tatizo kubwa la Afrika ni soko na kubadilisha fikra za vijana katika bara letu kwa  kupata ellimu juu ya namna   Watakavyoweza kujikwamua kiuchumi  hali itakayosadia kuondokana na umaskini uliokithiri hivyo ifike hatua watu wasiwe wanahitaji kupewa pesa pindi inapohitaji kupewa elimu "amesema Profesa Gabriel

  Amewataka wakufunzi wa vyuo kurudi vyuoni na kubadilisha mawazo ya vijana kurudi katika mtazamo chanya wa kujipatia maendeleo kuliko kusubiri kusukumwa na watu juu ya kupata ajira.
   Profesa Elisante Ole Gabriel akizungumza katika Mjadala huo
  washiriki wakimsikiliza Profesa Ole Gabriel
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Ukosefu wa Ajira ni Matokeo sio Janga barani Afrika-Profesa Ole Gabriel Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top