728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, November 8, 2016

  TMK Taarab kutambulisha mbili Alhamis

  BENDI ya muziki wa taarabu ‘Yah TMK Morden Taarab’ inafaya utambulisho wa nyimbo zake mbili za mwanzo, utakaofanyika Alhamis ya Novemba 10 mwaka huu.

  Akizungumzia na mtandao huu, Mkurugenzi wa bendi hiyo Said Fella, alisema kuwa utambulisho huo maalum utaanza katika vyombo vya habari kwa kuanza kupiga nyimbo hizo katika vituo vya hapa nchini.

  Alisema nyimbo mbili zilizomaliza kurekodiwa ambazo zimeimbwa na wanamuzi mahili ambao ni Mwanahawa Ali aliyeimba wimbo wa Sina Puma na Aisha Vuvuzela aliyeimba wimbo wa ‘Kibaya kina Wenyewe’ .

  Fella alisema bendi hiyo inayoundwa na wanamuziki mahili wa muziki huo , Mussa Mauji, Mussa Mipango, Omar Tego, Fatuma Nyoro, Mauwa Tego, Babu Kijiko na wengine waliopo kwenye bendi hiyo wanatoka kwenye kituo cha Mkubwa na wanawe ni pamoja na Mwanadada Jeza, pamoja na Hassan Dogo na Ibrahim.

  Alisema kuwa hata hivyo wataendelea kurekodi nyimbo nyingine na kuzitambulisha kama mwendelezo mpaka kufika uzinduzi wa albamu na bendi yao hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: TMK Taarab kutambulisha mbili Alhamis Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top