728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Saturday, November 19, 2016

  TaWaSaNet yawakutanisha wadau mbalimbali wa mazingira nchini


  Mtandao wa asasi za kiraia unaojihusisha na masuala ya Maji na mazingira Nchini (TaWaSaNet) umeandaa mkutano  uliowakutanisha wadau Mbalimbali wa Mazingira Nchini, ili kuadhimisha  wiki ya usafi wa Mazingira inayoenda sambamba na siku ya choo na kunawa mikono Duniani inayo adhimishwa novemba 19 ya kila mwaka.

  Akizungumza katika mkutano huo mgeni rasmi Naibu waziri wa Afya Jinsia wazee na Watoto Dkt Khamisi Kigwangala amesema, wizara yake imejipanga kusimamia kwa ukaribu  utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya  kitaifa na kimataifa inayolenga upatikanaji wa vyoo bora mashuleni na kwenye vituo vya Afya.

  Dkt Kigwangala ameipongeza Taasisi ya TaWaSaNet kwa kufanikisha na kuandaa mkutano huo kwa kuwa wadau wazuri wa mazingira na kuzitaka asasi nyingine za kiraia kuunga mkono jitihada za serikali ya Awamu ya Tano katika kuendeleza kampeni mbalimbali za usafi  hapa Nchini.

  Katika mkutano huo Kigwangala ametoa Tuzo kwa wanahabari mahiri kwenye uandishi wa makala usafi na mazingira ambapo  Bw.Gervas Hubile amepata tuzo ya makala bora ya usafi wa mazingira kwa upande wa radio na Bi Salome Gregory ametwaa tuzo ya Makala bora ya usafi wa mazingira kwa upande wa magazeti.

   Naibu waziri wa Afya Jinsia wazee na Watoto Dkt Khamisi Kigwangala akizungumza na wadau mbalimbali wa mazingira juu ya kutoa tuzo kwa wanahabari mahiri kwenye uandishi wa makala usafi na mazingira leo jijini Dar es Salaam.  
   .Afisa Sera wa Taasisi ya Tanzania Water and Sanitation Network (TAWASANET), Darius Mhawi wa (kwanza kushoto) akizungumza machache  kwenye utoaji wa tuzo kwa wanahabari mahiri kwenye uandishi wa makala usafi na mazingira leo jijini Dar es Salaam.
   Naibu waziri wa Afya Jinsia wazee na Watoto Dkt Khamisi Kigwangala akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali  leo jijini Dar es Salaam.picha na Yasir Adam wa Globu ya jamii.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: TaWaSaNet yawakutanisha wadau mbalimbali wa mazingira nchini Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top