728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Sunday, November 13, 2016

  TAIFA STARS YAFANYA MAZOEZI YA MWISHO,TAYARI KUKWAANA ZIMBABWE LEO.

  Leo Siku ya Jumapili November 13,2016 timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ itashuka dimbani kucheza na wenyeji Zimbabwe mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaochezwa kwenye uwanja wa Taifa wa Harare mjini Harare.

  Mchezo huo utachezwa majira ya saa tisa alasiri kwa saa za Zimbabwe wakati Tanzania itakuwa saa kumi jioni kwa saa za Afrika Mashariki na utakaoneshwa na kituo cha Televisioni ya Taifa ya Zimbabwe (ZBC) na hapa nyumbani wataungana na kituo cha Televisioni cha Azam TV.

  Wakiwa chini ya kocha Mkuu Boniface Mkwasa kikosi chote kimefanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa Harare na tayari kwa vita hiyo ya Kesho na ushindi wa kesho utakuwa na faida ya kuipandisha Tanzania katika viwango vya FIFA.

  Mchezaji wa timu ya Tanzania Mbwana Samatta ambaye pia anachezea timu ya Genk ya Ubelgiji akiwa na mchezaji mwenzake Thomas Ulimwengu wakijiandaa kwa mazoezi mjini Harare nchini Zimbabwe tayari kwa mchezo wao na timu ya Taifa ya Zimbabwe jumapili.
  wachezaji wa timu ya Taifa Taifa Stars wakijiandaa kwa mazoezi.
  Mchezaji Thomas Ulimwengu akibeba majiya kunywa kwenye toroli kwa ajili kunywa wakati wa mazoezi ya timu hiyo.
  Kocha Mkuu wa timu ya Taifa taifa Stars Boniface Mkwasa akijadiliana jambo na makocha wenzake.
  Mazoezi yakiendelea.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: TAIFA STARS YAFANYA MAZOEZI YA MWISHO,TAYARI KUKWAANA ZIMBABWE LEO. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top