728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, November 14, 2016

  Siku ya Kisukari Duniani- Muhimbili Yawapima Kisukari Wafanyakazi Wake LEO

   Dk Elias Mwandwani akimpima kisukari mmoja wa wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Leo.
  kik2
  Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akiwa amevaa beji ikiwa ni ishara ya kuwamasisha wafanyakazi wa hospitali hiyo kupima kisukari leo.
  kik3
  Juma Selemani akipima uzito Leo kabla ya kupima kisukari  katika Hospitali  hiyo leo.
  kik4
  Dk Faraja Chiwanga wa Muhimbili akimpima kisukari Juma Selemani katika hospitali hiyo Leo.
  …………………………………………………………….
   Na Neema Mwangomo
   
  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Leo imeadhimisha siku ya kisukari duniani kwa kuwapima kisukari wafanyakazi wa hospitali hiyo. 
   
  Leo wafanyakazi wa hospitali hiyo walikuwa wakipimwa  kisukari na uzito pamoja na kupatiwa ushauri jinsi ya kupunguza uzito kwa wale waliobainika kuwa na uzito mkubwa.
   
  Wafaanyakazi waliojitokeza  leo ni madaktari, wafanyakazi  kurugenzi za utawala, wauguzi  na wanafanyakazi mbalimbali wa hospitali hiyo.
   
  Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo Profesa Lawurence Museru alikuwa mstari wa mbele katika kuwashawishi wafanyakazi kupima kisukari.
   
  Naye Mkuu wa Kitengo cha Kisukari, Dk Mohamed J. Mohamed amesema Muhimbili imeona kuna umuhimu wa kupima kisukari kwa wafanyakazi wake kutokana na kubanwa na shughuli mbalimbali na hivyo mara nyingi wamekuwa wakikosa nafasi ya kupata huduma za afya.
   
  “Tumeona ipo haja ya kutoa huduma hii kwani kuwa mfanyakazi wa Muhimbili haimaanishi kwamba upo salama kiafya hivyo tunafanya hivi ili wapate nafasi ya kupia kisukari,” amesema Dk Mohamed.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Siku ya Kisukari Duniani- Muhimbili Yawapima Kisukari Wafanyakazi Wake LEO Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top