728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, November 28, 2016

  RAIS DKT MAGUFULI AMEAMUA KULETA MABADILIKO YA KWELI NA TUMUUNGE MKONO-ULEGA

   Mbunge wa mkuranga Mh Abdala Ulega akimkabidhi Pikipiki Mwenyekiti wa vianz Bw Rashid Gadaf . Picha zote na Yasir Adam Blogu ya Jamii.

   Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Mh Abdala Ulega akizungumza na wajumbe wa Halmashaur kuu kupitia chama cha CCM kata ya vianzi wilayani Mkuranga ,Wakati huohuo Mh.Ulega  alikabidhi Pikipiki Kwa Viongozi wa  Chama cha Mapinduzi CCM Kata  Viazi Mara baada ya kualikwa Kwenye mkutano wa ndani wa  Halmashauri kuu  ya CCM  Kata hiyo.
  Diwani wa Kata ya Vianzi akizungumza na wajumbe ya Halmashaur kuu wa kata ya vianzi kupitia chama cha Ccm wilayani mkuranga
  Mwenyekuti wa Kata ya Vianzi Bw Rashid Gadafi akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu kutoka chama cha Ccm wilayani mkuranga


  MBUNGE wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega amewataka vijana wa Chama cha Mapinduzi kujitokeza Kwa wingi katika uchaguzi Mkuu ujao wa Chama unaotarajia kufanyika mapema mwakani 2017.

  Amesema kuwa wanatakiwa kujitokeza Kwa wingi ili kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani Chama na lengo hasa kutaka kumsaidia Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa Ambaye ni rais wa Tanzania Dkt John Magufuli katika kutekeleza majukumu Yake.

  Akizungumza na Halmashauri kuu ya CCM kata ya Viazi Jana wilayani humo .alisema kuwa Kwa Dkt.Magufuli hakuna jambo la uzoefu kwake yeye ni Kazi tu.nakudai watu walidhani wimbo wa mabadiliko Kwa Dkt. Magufuli ilikuwa ni mzaha na sasa namba inasomeka kweli.

  "Mkitaka kujuwa Kuwa rais Dkt.Magufuli hakuna uzoezi angalieni Leo anachofanya Paul Makonda Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Kazi anayoifanya nikijana ambaye ametoka chuo juzi na akaaminiwa na wakubwa Leo anapiga Kazi hivyo lazima vijana tujiamini "alisema Mbunge Ulega.

  Akizungumza na Halmashauri kuu ya Kata ndani ya CCM alitumia mkutano huo kuwapongeza Kwa Kazi kubwa ya kukipambania Chama ambayo waliifanya katika Uchaguzi ulimalizika mwaka 2015.

  Alisema kutokana na Kazi hiyo kubwa ambayo wameifanya yeye kama Mbunge ameamua kutoa Zawadi Kwa Kata Kumi ambazo kiukweli waliongoza Kwa kukipa kura nyingi Chama cha Mapinduzi CCM hivyo ameamua kutoa zawaidi ya Pikipiki.

  Mbunge Ulega aliwasisitiza wanaCCM kuhakikisha wanamuunga mkono Kwa asilimia mia moja Rais Dkt.Magufuli ambaye amedhamiria kuwatumikia watanzania kivitendo.

  "Lazima tufanye Kazi ya kuwatimikia watanzania na hasa kutimiza ahadi zetu ambazo tulizitoa Kwa wananchi ili hata tutakaporudi mwaka 2020 ili iwe kazi nyepesi kuwaambia wananchi kwamba tumetekeleza moja mbili Tatu."alisema Ulega

  Aidha aliwataka wanaCCM kuondoa fitina na majungu katika kipindi hiki bali kazi iliyokuwa mbele ni kuchapa Kazi Kwa ajili ya wananchi na si vinginevyo.

  Ulega pia aliwaeleza makada hao wa Chama cha Mapinduzi aliwahakikishia kuwa hadi kufikia mwaka 2020 kushirikiana na wanaCCM kujenga Ofisi za Kata ndani Chama
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: RAIS DKT MAGUFULI AMEAMUA KULETA MABADILIKO YA KWELI NA TUMUUNGE MKONO-ULEGA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top