728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, November 10, 2016

  Rais Dkt John Pombe Magufuli kuongoza shughuli za kuaga mwili wa Marehemu Joseph Mungai viwanja vya Karimjee leo jijini Dar
  Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza kwa niaba ya Serikali.Shughuli za kuaga zitaongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli ambaye tayari amekwishawasili ukumbini hapo na kufuatiwa na viongozi wengine waandamizi wa chama na Serikali.

  Marehemu Mungai amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi na utumishi katika Chama na Serikali. Alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Mkuu wa Mkoa, Mbunge kuanzia miaka ya 1970 hadi 2010, na amekuwa Waziri katika wizara mbalimbali za Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuanzia Awamu ya kwanza mpaka ya nne.

  Viongozi Wastaafu kushoto ni Rais Mstaafu awamu ya pili Mh.William Benjamin Mkapa pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu awamu ya Pili Mh.Frederick Sumaye na viongozi wengine waandamizi wakiwa tayari kwa kuanza kuaga mwili wa marehemu Joseph Mungai ndani ya ukumbi wa Karimjee jijini Dar.

  Viongozi Wastaafu mbalimbali wakiwa tayari kwa kuanza kuaga mwili wa marehemu Joseph Mungai ndani ya ukumbi wa Karimjee jijini Dar.

  Nyimbo mbalimbali za maomboleza zikiendelea

  Ndugu,jamaa na Marafiki wakiendelea kuwasilika ukumbi wa Karimjee kwa ajili ya kuaga mwili wa Marehemu Joseph Mungai, Mbunge mstaafu wa Jimbo la Mufindi aliyefariki Novemba 08, 2016 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam..
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Rais Dkt John Pombe Magufuli kuongoza shughuli za kuaga mwili wa Marehemu Joseph Mungai viwanja vya Karimjee leo jijini Dar Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top