728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, November 10, 2016

  PROGRAM YA KUKUZA AJIRA ZENYE STAHA JIJINI DAR ES SALAAM YAFANIKIWA KUSAIDIA VIJANA KUANZISHA BIASHARA ZAO NA KUAJIRIKA

   Mratibu wa Mafunzo ya Ujasiriamali, katika  Program ya kukuza Ajira zenye Staha Jijini Dar es Salaam (YEID) Bw. Dominic Ndunguru akifafanua jambo alipokuwa akiwasilisha ripoti maalumu ya mrejesho wa namna mafunzo ya ujasiriamali yalivyosaidia kukuza ajira kwa vijana, leo Jijini Dar es Salaam.
  b4
  Mratibu wa Program ya kukuza Ajira zenye Staha jijini Dar es Salaam (YEID) katika upande wa kujengea uwezo vijana wa kuajirika, Bw. Avitus Mushumba akielezea akifafanua jambo wakati wa mkutano wa tano wa tathmini ya maendeleo ya program hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Don Bosco Youth Center leo Jijini Dar es Salaam.
  b5
  Meneja wa Program kutoka Jukwaa la Ushirikiano wa Kimataifa (FIC) la nchini Denmark Bi. Annette Larsen akitoa muelekeo wa namna watakavyo endelea kusaidia uendeshaji wa Program ya Kukuza Ajira zenye Staha Jijini Dar ers Salaam kwa awamu ya pili, program inayotarajiwa kuanza mapema mwezi wan ne mwakani.
  b1
  Afisa Msimamizi wa Program ya kukuza Ajira zenye Staha jijini Dar es Salaam (YEID) Bi. Emiliana Muchu akielezea kwa ufupi historia ya program hiyo wakati wa mkutano wa tano wa kutathmini maendeleo ya mradi huo leo Jijini Dar es Salaam.
  b2
  Mratibu wa Ushawishi na Utetezi, katika  Program ya kukuza Ajira zenye Staha jijini Dar es Salaam (YEID) Bw. Elly Ahimidiwe akielezea akielezea mafanikio ya utekelezaji wa Mikutano ya kutoa taarifa kuhusu mfuko wa Vijana na Baraza la Taifa la vijana, wakati wa mkutano wa tano wa tathmini ya maendeleo ya program hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Don Bosco Youth Centre leo Jijini Dar es Salaam.

  b6
  Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Bw. Godfrey Nyaisa akifafanua jambo katika mkutano wa tathmini ya utekelezaji wa Program ya Kukuza Ajira zenye Staha Jijini Dar es Salaam uliofanyka leo katika ukumbi wa Don Bosco Youth Center Dar es Salaam. Program hiyo ya miaka mitatu kwa awamu ya kwanza inatarajiwa kukamilika mapema mwishoni mwa mwaka huu, huku awamu ya pili ikitarajiwa kuanza mwezi Aprili 2017.
  b7
  Baadhi ya washiriki wa mkutano wa tathmini ya utekelezaji wa Programu ya Kukuza Ajira zenye Staha Jijini Dar es Salaam(YEID) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Don Bosco Youth Center  leo Jijini Dar es Salaam.
  Picha na: Frank Shija,MAELEZO.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: PROGRAM YA KUKUZA AJIRA ZENYE STAHA JIJINI DAR ES SALAAM YAFANIKIWA KUSAIDIA VIJANA KUANZISHA BIASHARA ZAO NA KUAJIRIKA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top