728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, November 10, 2016

  MOTO MKUBWA WATEKETEZA BOHARI LA KAMPUNI YA 7 GENERAL ENTERPRISES MIKOCHENI JIJINI DAR ES SALAAM


  Hivi ndivyo moto mkubwa ulivyokuwa ukiwaka katika Bohari la 7 General Enterprises ambapo walikuwa wakihifadhia Mataili, mchana eneo la Mikocheni Jijini Dar es salaam.

  Vikosi mbalimbali vya zima moto kutoka Serikali na Makampuni binafsi wakiendelea na juhudi za kuuzima moto huo.

  Baadhi ya watu mbalimbali wakiendelea kushuhudia tukio hilo la kuteketea kwa Bohari

  Moto Mkubwa ukiendelea kuwaka


  Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi wa Kinondoni Suzan Kaganda akizungumzia kwa ufupi tukio hili na kusema kuwa kwa sasa hawezi zungumza chochote mpaka moto utakapozimwa kabisa


  Hapa mpaka Trekta nalo lilihusika katika kuhakikisha moto huo unazimika

  Mmoja wa waandishi wa Habari ambaye hakujulikana anatokea katika chombo gani akiwa anaendelea kutafuta sehemu nzuri ya kuchukua taarifa.

  Baadhi ya wataalam wa kuzima moto wakiwa wanaendelea na juhudi za kutazama maeneo ambayo moto unawaka zaidi ili kuuzima

  Moja ya Gari la zima moto likiwa linawahi eneo la Tukio kusaidia kuzima moto
  Zima moto wakiendelea na shughuli ya kuhakikisha moto unazimika katika Bohali hilo

  Moto ukiendelea kuteketeza Bohari hilo lililokuwa la kuhifadhia mataili

  Pamoja na watu kupewa tahadhali ya Moto mkubwa uliokuwa unawaka lakini bado walikuwa wakiongezeka kushuhudia tukio hilo.

  Katika juhudi za kuhakikisha moto huo unazimika kabisa magari ya kila aina yanayobeba maji yalichukuliwa kuongeza nguvu za kuzima moto huo.

  Ulinzi ukiwa umeimarishwa kabisa katika eneo ambalo moto ulikuwa unawaka

  Mmoja wa wafanyakazi wa Bohari hilo Shaban Salum akielezea kwa ufupi kile alichokiona wakati moto huo unaanza kuwaka mida ya saa sita mchana  Magari ya zimamoto na mengine ambayo ni ya kubebea maji yakiwa katika eneo la Bohali la 7 General kuhakikisha wanashirikiana kumaliza moto huo


  Umati wa watu wakiwa katika eneo hilo la Bohari wakiendelea kushuhudia Tukio hilo

  Watu wengine wakiwa wamekaa Jirani kabisa na Moto huo bila wasiwasi wakishuhudia tukio hilo la Moto.
   
  Taarifa kamili itakuja kutoka Jeshi la Polisi
  Picha zote na Fredy Njeje/Blogs za mikoa
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MOTO MKUBWA WATEKETEZA BOHARI LA KAMPUNI YA 7 GENERAL ENTERPRISES MIKOCHENI JIJINI DAR ES SALAAM Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top