728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, November 29, 2016

  Manyanya:Foundation sio sifa ya mtu kujiunga chuo kikuu

  Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi(Kushoto),Eng.Stella Manyanya akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam,Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ya Elimu,Prof.Simon Msanjila

  Na Chalila Kibuda.

  Kozi za foundation katika  vyuo  zinazotolewa sio mfumo wa Elimu uliopangwa na serikali kumfanya aliyepita kuwa na sifa ya kujiunga na chuo kikuu.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Naibu Waziri Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya amesema kozi za foundation  katika vyuo haijawekewa mfumo ambao unatambulika.

  Mhandisi Stella amesema utaratibu  huo vyuo vimefanya vyenyewe hivyo serikali haiwezi kuukubali mfumo elimu hiyo.

  Amesema anaesoma foundation apewe cheti na kama atahitaji  kujiendeleza asafishe cheti au asome mfumo ambao utamfikisha katika shahada.
  Amesema suala la watu waliosoma cheti kisha diploma na wakajiunga chuo kikuu hawako sahihi kutokana na vyeti hivyo.Amesema serikali inafanya maboresho ya elimu nchini kutokana na kibaoni vitu vingi ambavyo vimetokana na watu kwenda tofauti na mfumo wa elimu uliowekwa.

  Stella amesema wanaendelea kufanya maboresho katika diploma ya ualimu kuweza kuiondoa.Aidha amesema kuwa serikali haitaruhusu elimu kuwa holela kwa watu kuwa tofauti na mfumo uliowekwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Manyanya:Foundation sio sifa ya mtu kujiunga chuo kikuu Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top