728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, November 16, 2016

  JAJI MKUU MGENI RASMI MASHINDANO YA GOLF YA WAITARA TROPHY


  Na Luteni Selemani Semunyu


  JAJI Mkuu wa Tanzania Mh Othman Chande anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika mashindano ya gofu ya Mkuu wa Majeshi mstaafu Generali Geogre Waitara maarufu Waitara Trophy 2016. 

  Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Klabu ya Golf ya Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania ya Lugalo wanaoandaa mashindano hayo Brigedia Jenerali Michael Luwongo wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar Es salaam. 

  Brigedia Jenerali Luwongo alisema maandalizi yamekamilika na yanatarajiwa kufanyika Jumamosi Novemba 19 na kushirikisha Wachezaji wa makundi yote isipokuwa watoto huku klabu zote zikithibitisha kushiriki.
  “Tumeshajiandaa vya kutosha na wadhamini wametuwezesha na mwitikio mpaka sasa ni mkubwa na tayari wachezaji 150 wametibitisha kushiriki mashindano haya yanayodhaminiwa na kampuni ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha John Walker red label” Alisema Generali Luwongo. 

  Aliongeza kuwa mbali na Vilabu wenyeji klabu ya Lugalo ,Gymkhana Dar es Salaam,Gymkhana Morogoro ,Gymkhana Arusha, Kili,na TPC Moshi ,na Mufindi pia kutoka Arusha Mkuu wa majeshi Mstaafu Mirisho Sarakikya amethibitisha kushiriki katika mashindano hayo. 

  Pia alisema Wanatarajia kuongea na Chama cha Golf Nchini ili kuona namna gani baadhi ya Mashindano ya Ndani ikiwemo hili la Waitara kuwa na hadhi ya Kimataifa kutokana na kuwa mashindano hayo na hamasa kubwa iliyopo. 

  Kwa upande wake Nahodha wa Klabu ya Lugalo Kapten Japhet Masai alisema mashindano hayo yatakuwa ya Stroke play Net ambapo yatatanguliwa na Wachezaji wa Kulipwa na Wachezaji wasaidizi siku ya Ijumaa Novemba 18 huku siku inayofuata yakifanyika kwa makundi yaliyosalia. 

  Naye Meneja wa mawasiliano wa Serengeti Abbas Abraham alisema maandalizi ya zawadi ikiwemo ya Vikombe yamekamilika na wanachosubiri ni zoezi la kukabidhiwa kwa Washindi. 

  Mashindano ya Kombe la Waitara yanayofanyika kila mwaka ikiwa ni kumbukumbu ya kutambua mchango mkubwa uliotolewa na mkuu huyo wa majeshi katika kuanzisha Uwanja wa Golf wa Lugalo Mwaka 2006.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: JAJI MKUU MGENI RASMI MASHINDANO YA GOLF YA WAITARA TROPHY Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top