728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, November 9, 2016

  Jaji Lubuva atoa nasaha kwa menejimenti ya NEC

  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) JajiMstaafu Damian Lubuvaakizungumza na wajumbe wa kikao cha menejimenti ya tume hiyo (hawapopichani) jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Bwana Kailima Ramadhani.Picha na Christina Njovu, NEC.

  ……………………………………………

  Mwenyekiti Lubuva alitoa nasaha hizo katika Kikao cha Utawala kinachoongozwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi ambacho hufanyika kila wiki kwa ajili ya kuimarisha utendaji kazi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

  Amesema kuwa kuzingatia nidhamu katika kazi kutawasadia sio tu katika kutekeleza majukumu ya Tume bali mahali popote ambapo mfanyakazi atapelekwa. Aidha Mwenyekiti Lubuva amemewashukuru wakuu hao wa Idara mbalimbazi za Tume kutokana na ushirikiano waliounyesha wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

  “Nakushukuru Mkurugenzi wa Uchaguzi na timu unayoiongoza kwa jinsi mlivyofanya kazi kama timu na kuweza kufanikisha Uchaguzi Mkuu uliopita najivunia kufanya kazi nanyi” Aidha napenda kusisitiza nidhamu ya kazi kwa viongozi na wafanyakazi kuwa ni muhimu sana katika kuleta ufanisi wa kazi sio tu katika Tume bali mahali popote ambapo mfanyakazi atapelekwa.

  Amewasihi wasipende kusukumwa kufanya kazi na kwamba katika kutekeleza hilo mtu yeyote anatakiwa kujipanga na kuwa tayari kufanya kazi ikiwa ni pamoja na kuwahi mahali pa kazi na kutimiza wajibu wake kwa ufanisi. Pia amesisitiza suala la kuwa na uaminifu katika kazi ikiwa ni pamoja na masuala ya kijamii kwa ujumla ambapo kutokana na hilo wananchi wataweza kuiamini taasisi nzima..

  “Kama mlivyofanikisha uchaguzi uliopita fanyeni kazi kwa kujituma sio tu katika Uchaguzi uliopita bali kwa kazi zilizopo na kazi zinazokuja ambapo kazi zilizopo mbele yetu ni nyingi na kubwa.” Alisema Mwenyekiti Jaji Lubuva na kufafanua kuwa. “Kama mlivyofanikisha Uchaguzi Mkuu uliopita pia fanyeni kazi kwa bidii kwa maandalizi ya chaguzi zijazo kwa ufanisi na nidhamu”

  Pia mkiheshimiana kati yenu itawawezesha kufanya kazi kwa nidhamu kwa kufuata taratibu zilizowekwa ili kufanikisha shughuli zilizopo mbele yetu. Akitoa neno la shukrani Mkuu wa Idara ya Huduma za Kisheria Bwana Emmanuel Kawishe amemshukuru Mwenyekiti Jaji Lubuva kwa namna alivyowaongoza na kufanikisha Uchaguzi Mkuu uliopita.

  Bwana Kawishe amemuahidi Mwenyekiti kwa niaba ya viongozi na wafanyakazi wenzake kuwa watatekeleza yale aliyowaasa na kumpongeza kwa kufuata sheria wakati wa Uchaguzi mkuu uliyopita.

  Kikao hicho ni miongoni mwa vikao vinavyofanyika kila wiki kwa lengo la kuleta ufanisi katika utendajikazi katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi.Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Damian Lubuva amewasihi viongozi na wafanyakazi wa tume hiyo kuzingatia nidhamu ya kazi ili kuleta ufanisi katika kutekeleza majukumu yao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Jaji Lubuva atoa nasaha kwa menejimenti ya NEC Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top