728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, November 14, 2016

  JAJI KIONGOZI ATEMBELEA MAHAKAMA KUU KANDA YA BUKOBA

  Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali (wapilikushoto) akiwa ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu, Mhe. Salum Kijuu alipomtembelea ofisi kwa Mkuu wa Mkoa huyo kumpa pole kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera mnamo tarehe 10.09.2016 na kusababisha maafa katika baadhi ya miundombinu mkoani huo, Mahakama Kuu ikiwa mojawapo. Kulia ni Mhe. SalvatoryBongole, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu- Kanda ya Bukoba.
  Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali, (wa pili kulia) akikagua jengo la Mahakama Kuu, Kanda ya Bukoba ambalo lilipata mipasuko ‘minor cracks’ kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera. Pamoja ni Jaji Kiongozi, wa pili kushoto ni Mhe. Jaji Matogoro, Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Bukoba, wa nne kushoto ni Mhe. Ilvin Mugeta, Msajili- Mahakama Kuu ya Tanzania ambaye aliambatana na Mhe. Jaji Kiongozi katika ziara yake Mkoani humo.
  Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba, Mhe. Salvatory Bongole, akiongea kitu mbele ya Watumishi wa Mahakama, Kanda ya Bukoba kabla ya kumkaribisha rasmi Mhe. Jaji Kiongozi kuongea na Watumishi wa Mahakama wa Kanda hiyo mara baada ya kukagua jengo la Mahakama lililopata maafa kufuatia tetemeko la ardhi.
  Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba, Mhe. Salvatory Bongole, akiongea kitu mbele ya Watumishi wa Mahakama, Kanda ya Bukoba kabla ya kumkaribisha rasmi Mhe. Jaji Kiongozi kuongea na Watumishi wa Mahakama wa Kanda hiyo mara baada ya kukagua jengo la Mahakama lililopata mipasuko kufuatia tetemeko la ardhi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: JAJI KIONGOZI ATEMBELEA MAHAKAMA KUU KANDA YA BUKOBA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top