728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, November 24, 2016

  INTRODUCING NEW SINGLE "NJOO BAADAYE" BY COYO

  Baada ya kuachia video/wimbo wake wa kwanza ‘NOMA’ miezi michache iliyopita, msanii Coyo ambaye ni mwenyeji wa jiji la miamba, Mwanza anatambulisha kazi yake mpya NJOO BAADAE, ikiwa ni ya pili kuachiwa akiwa chini ya usimamizi wa Tetemesha Entertainment. 
  Akizungumzia wimbo wake mpya, Coyo anasema, “NJOO BAADAE ni wimbo unaozungumzia maisha ya kila siku ya vijana”.“Ninamzungumzia mtu anayekuchanganyia mafaili kwa stori (umbea) muda ambao unamishe zako ambazo haziendani na stori  zake, hivyo unaamua kumchana habari hizo apeleke kwa zinaowahusu au aje baadae.” Ameongeza. 
  NJOO BAADAE imeandikwa na Coyo ambaye pia amefanya viitikio vya kuimba, na muziki wake umeandaliwa na watayarishaji watatu, Mr T Touch, mtayarishaji mpya aitwaye Daydream pamoja na KidBway chini ya usimamizi wa Tetemesha Ent.
                                                               
  Wimbo wa NJOO BAADAE pamoja na Instrumental vimeambatanishwa hapa, share na wengine kadri uwezavyo.       
  Tazama video yake iliyopita ‘NOMA’ hapa: https://youtu.be/VEPUTJL_Tj8

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: INTRODUCING NEW SINGLE "NJOO BAADAYE" BY COYO Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top