728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, November 2, 2016

  HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM YAKANUSHA KUTOA ZABUNI KWA KAMPUNI AMBAZO HAZINA SIFA


  Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam,Mussa Kafana akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu kuwepo kwa taarifa ambayo inadai kuwa Halmashauri hiyo imetoa zabuni kwa Kampuni ambazo hazina sifa.


  Na Bakari Madjeshi,Globu ya Jamii 

  Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imekanusha taarifa ya kutoa Zabuni kwa Kampuni ambazo hazina vigezo kupata zabuni hizo. 

  Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam,Naibu Meya wa Halmashauri hiyo,Mussa Kafana amesema kumekuwepo na taarifa ikidai kuwa Halmashauri hiyo imetoa zabuni kwa Kampuni ambazo hazina sifa. 

  "Tumeona tutoe ufafanuzi kwamba hatujatoa zabuni kwa Kampuni ambayo haina sifa,Mfano Kenya Airport ambayo mpaka leo mkataba wake haujasainiwa,"amesema Kafana 

  Amesema baadhi ya mikataba haijasainiwa kutokana na Kampuni hizo kutotimiza vigezo na masharti vinavyotakiwa kama zabuni inavyoeleza. 

  Kafana ameeleza kuwa Mikataba haijasainiwa kutokana na Kitabu cha Zabuni kinaonyesha kuwa Halmashauri ya Jiji kitu gani inataka ikiwa ni pamoja na kutimiza Masharti hayo ya Halmashauri ya Jiji. Pia amesema Mzabuni anatakiwa kuleta dhamana ya Asilimia 10 ya kile kiwango alichobidi katika kuomba zabuni,hiyo ikiwa ni kwa mujibu wa Kitabu cha Zabuni katika sura ya 41 Kifungu cha kwanza
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM YAKANUSHA KUTOA ZABUNI KWA KAMPUNI AMBAZO HAZINA SIFA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top