728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, November 21, 2016

  HAKI ELIMU YAISHAURI SERIKALI KUHARAKISHA UUNDAJI WA BODI YA KITAALAMU YA WALIMU

  Na Anthony John,Globu ya Jamii

  Shirika lisilo la Kiserikali linalojihusisha na Elimu nchini, HAKI ELIMU limeishauri Serikali kuharakisha uundaji wa bodi ya kitaalamu ya Walimu ili kusaidia kuweka na kubaini viwango bora vya taaluma ya Ualimu.

  Ushauri huo,umekuja baada mapema mwezi huu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ufundi kutoa waraka Na.5 wa Mwaka huu 2016 unaoleta Mabadiliko kadhaa katika program za Mafunzo ya Ualimu nchini.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi mtendaji wa shilika Hilo la HAKI ELIMU, John Kalage amesema miongoni mwa Mabadiliko hayo ni kwenda mamlaka ya usimamizi wa Elimu ngazi ya Cheti na stashahada kutoka NACTE na kuyarudisha wizarani chini ya uangalizi wa baraza la mitihani NECTA.

  Kalage amesema kuwa kwamujibu wa waraka huo programu za Mafunzo ya Ualimu zitakuwa Astashahada Cheti, na stashahada , Diploma Mafunzo taraji ya stashahada ya juu ya Elimu sekondari yalikuwa yakitolewa kuanzia Mwaka wa masomo 2014/15 yamesitishwa.

  "Wizara ya Elimu ndio itakuwa ikitoa maelezo ya sifa za kujiunga na Mafunzo ya Ualimu, Necta itakuwa inasimamia Mafunzo ya Ualimu huku ikitahini na kutoa tuzo", amesema Kalega.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Haki Elimu,John Kalage katikati akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya kuishauri Serikali kuharakisha uundaji wa bodi ya kitaalamu ya Walimu ili kusaidia kuweka na kubaini viwango bora vya taaluma ya Ualimu.Kulia ni Meneja Habari na Utetezi-Haki Elimu,Elisante Kitulo,Kutoka Kushoto ni Maneja Udhibiti Ubora Haki Elimu,Robert Mihayo
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: HAKI ELIMU YAISHAURI SERIKALI KUHARAKISHA UUNDAJI WA BODI YA KITAALAMU YA WALIMU Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top