728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, November 9, 2016

  Etihad yazindua safari za Johnnesburg kwa kutumia ndege ya kisasa aina ya Boeing 787 Dreamliner.

  Ndege ya Shirika la Etihad ya Boeing 787-9 ikiwasili kwenye uwanja wa ndege wa O.R Tambo jijini Johnnesburg.

  SHIRIKA la Ndege la Etihad kupitia ndege yake ya Boeing 787 Dreamliner limeanzisha safari zake mpya katika Jiji la Johnnesburg kuanzia tarehe 01 Novemba 2016 mchana kwa uzinduzi wa ndege hiyo kutoka Abu Dhabi.

  Ndege hiyo iliondoka Abu Dhabi saa 4:15 asubuhi na ilitarajiwa kuwasili saa 10:45 jioni. Pia ilitarajiwa kuondoka Jonhnnesburg 1:50 jioni na kuwasili Abu Dhabi saa 12: 10 asubuhi kesho yake.

  Ndege hiyo ya kisasa ya Etihad inayotoa huduma kwa madaraja ya kwanza na kawaida inatarajiwa kutoa huduma za kila siku katika jiji hilo…Afisa Mkuu Mtendaji wa Shirika la ndege la Etihad, Peter Baumgartner alisema, “Uamuzi wa kutumia ndege hiyo ya kisasa zaidi kwa safari za Johnnesburg umelenga kukidhi mahitaji halisi ya wateja kutokana na ongezeko la idadi ya watu wanaohitaji huduma za daraja la kwanza na huduma bora kwa wanaokwenda na kutoka nchini Afrika Kusini.
  Wasafiri wanaokwenda na wakati wanahitaji huduma nzuri, zenye ubunifu na salama, na matarajio yetu ni kutoa huduma zenye kiwango cha juu cha ubora zinazokidhi ukarimu na teknolojia ya hali ya juu ili kuifanya safari yako iwe ya kukumbukwa.”

  Mkurugenzi wa Shirika la ndege la Etihad nchini Afrika Kusini aliongeza kuwa, “Kuanzishwa kwa ndege ya Boeing 787 kutaongeza maendeleo kwa kuvutia wageni wengi kutumia safari hizo. Ndege hii yenye ubora wa hali ya juu ina kila huduma ndani yake na mandhari ya kuvutia.”

  Ndege hiyo ya kisasa imeundwa ikiwa na vitu mbalimbali ndani yake vitakavyokufanya uburudike na kusafiri kwa uhuru zaidi. Kuna vituo takriban 28 kwa daraja la kwanza na kuna vituo vyenye ubora 271 kwa ajili ya daraja la kawaida.
  Kwa daraja la kwanza kuna huduma ya vitanda vyenye ukubwa wa kutosha na nafasi ya kutosha ya mtu kuburudika. Kuna vitambaa laini na vyenye kuvutia ambavyo vimezungushiwa kwenye kila kiti. Huku kukiwa na mfumo wa kielektroniki unaomwezesha mteja kusogeza kiti kwa kiwango anachotaka jambo linalompa uhuru zaidi akiwa safarini.

  Kila chumba kwenye daraja la kwanza kuna runinga kubwa ya flat screen unayoweza kutumia kwa njia ya kugusa huku ukipata huduma ya vifaa vya kudhibiti kiwango cha kelele,

  Vilevle hata kwenye daraja la kawaida kila kiti kina runinga ndogo pamoja na vifaa vya kusikilizia redio kwa wateja wanapokuwa safarini. Pia kuna viti vikubwa ambavyo vinamfanya mteja kuwa huru kuweka miguu kwa kadri anavyotaka.
  Aidha kuna mfumo unaowawezesha wateja kutumia intaneti bure huku kukiwa na mahali ambapo abiria anaweza kuchomeka USB yake ili kuchaji simu na huduma zingine za kimawasiliano. Muda wote unapokuwa kwenye ndege hiyo utaburudika kwa kupata chaneli mbalimbali ambazo zinaonekana katika ubora wa hali ya juu huku wahudumu wakitoa huduma zilizotukuka kwa wateja.

  Wahudumu wa ndege waliopo ni wabobezi kutoka vyuo vikubwa vinavyotambulika ulimwenguni kama vile Flying Nannies waliopata mafunzo Norland College nchini Uingereza kuhusuna na malezi ya watoto wanapokuwa kwenye ndege.

  Pia kuna wasimamizi wa vyakula waliobobea ambao wamefanya kazi katika hoteli kubwa na maarufu duniani huku wakiwa na mafunzo ya kuhudumia daraja la kwanza ikiwa ni pamoja na kuwa na ujuzi wa kuandaa vinywaji laini.

  Wateja wanaotumia ndege hiyo watapata fursa ya kufurahia kuona mandhari ya nje kupitia madirisha makubwa na uwapo wa hali ya hewa tulivu.

  Shirika la ndege la Etihad limekuwa na utaratibu wa kuwasaidia wasafiri wake wanaotoka Afrika wanapofika kwenye mamlaka ya forodha nchini Marekani na Uwanja wa Ndege wa Abu Dhabi kukamilisha utaratibu wa wahamiaji kwa haraka.

  Utaratibu huu ukiacha Shirika la Ndege la Etihad ukanda wa ghuba, inawapa fursa wateja kukamilisha taratibu zote muhimu za uhamiaji, ushuru na forodha pamoja na kushughulikia vibali vya usalama kwa wasafiri wanapofanya safari kati ya Abu Dhabi na Marekani jambo linalowawezesha kupunguza mlolongo mrefu wanapowasili katika uwanja wa ndege wa Marekani.

  Jiji la Johnnesburg ni mji wa tisa kuhudumiwa na ndege aina ya B757-9 Dreamliner. Ndege hiyo pia inatoa huduma katika miji ya Brisbane, Düsseldorf, Perth, Riyadh, Shanghai, Singapore, Washington DC and Zurich.

  Ratiba ya ndege ya Dreamliner kutoka Abu Dhabi – Johannesburg:
  Ndege No.
  eneo
  Kuondoka
  Eneo
  Kuwasili
  Kipindi
  EY604
  Abu Dhabi
  10:15am
  Johannesburg
  4:45pm
  Daily
  EY603
  Johannesburg
  7:50pm
  Abu Dhabi
  6:10am (+1)
  Daily

  Muda wa kuondoka umeorodheshwa kulingana na muda wa eneo husika.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Etihad yazindua safari za Johnnesburg kwa kutumia ndege ya kisasa aina ya Boeing 787 Dreamliner. Rating: 5 Reviewed By: MICHUZI BLOG
  Scroll to Top