728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, November 9, 2016

  CCM YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA MHE. MUNGAI


  Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Abdulrahman Kinana amemtumia salamu za rambi rambi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Ndg. Jesca Msambatavangu kufuatia kifo cha Mhe Joseph Mungai, Mbunge mstaafu wa Jimbo la Mufindi kilichotokea jana tarehe 08 Novemba, 2016 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.

  Mhe. Mungai, ameshika nyadhifa mbalimbali za uongozi na utumishi katika Chama na Serikali. Alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Mkuu wa Mkoa, Mbunge kuanzia miaka ya 1970 hadi 2010, na amekuwa Waziri katika wizara mbalimbali za Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuanzia Awamu ya kwanza mpaka ya nne.

  Mhe. Mungai, atakumbukwa na wanaCCM, na wananchi wa Mkoa wa Iringa na Tanzania kwa kuasisi na kuendeleza shamba kubwa la miti la SAOHILL na kwamba mchango wake huo tutaendelea kuuenzi na kuuthamini.


  Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe. 
  Imetolewa na:- 

  Christopher Ole Sendeka (MNEC)
  MSEMAJI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: CCM YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA MHE. MUNGAI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top