728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, November 28, 2016

  BENKI YA UBA YATOA MSAADA PUGU SEKONDARI

  Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii

  Benki ya United Bank of Africa (UBA), jana imetoa msaada wa viti, Magodoro, Magongo ya kutembelea na vitabu vya kujisomea kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu ya shule ya sekondari ya wavulana Pugu jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza wakati wa kutoa vifaa hivyo, Meneja wa benki hiyo nchini ,Peter Makao, amesema kuwa wamechagua kutoa vifaa hivyo katika shule hiyo kutokana na mahitaji ya watoto hao ambao wamekuwa wakisoma katika mazingira magumu.

  “Vitu hivi ambavyo tumevitoa leo vitasaidia kwa kiasi kikubwa kuwapunguzia watoto hawa wenye mahitaji maalum kusoma kwa mawazo kwa kujiona kwamba wao ni sehemu hii ya shule kwa kupata mahitaji yao wote kama ilivyo kwa wengine”Amesema Makao 

  Ametoa wito kwa wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili waweze kufanikiwa katika jamii na baadae wajivunie kuwa walisoma pugu .
  Wanafunzi wa Pugu sekondari wakishusha kwenye gari vifaa vilivyokabidhiwa na benki ya UBA kwa ajili ya wanafuzni wenye mahitaji maalum
  Mkurugenzi mkuu wa Benki ya UBA,Peter Makao akiwa na Meneja Operesheni Omary wakikabidhi mafuta ya ngozi kwa kijana mwenye ulemavu wa ngozi ,Daudi Nyangusi na Meneja ufadhili wa eleimu kutoka TEA , Tito Mganwa.
  Mkurugenzi mkuu wa Benki ya UBA,Peter Makao akiwa meneja operesheni Omary wakikabidhi vitabu kwa wanafunzi Salum Mohamed na Ramadhani Juma pamoja na Meneja ufadhili wa eleimu kutoka TEA , Tito Mganwa.
  Wafanyakazi waUnited Bank of Afrika wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wenye ulemavu wa shule ya Sekondari ya wavulana pugu jijini Dar es Salaam.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: BENKI YA UBA YATOA MSAADA PUGU SEKONDARI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top