728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, November 25, 2016

  Baraza la Madiwani Lamfukuza Kazi Mtumishi.


  Na. Immaculate Makilika - MAELEZO

  BARAZA la Madiwani ya Halmashauri ya Mji wa Bunda limemfukuza  kazi  Bw. Eliud Haonga aliyekuwa mtumishi wa Idara ya Ardhi na Mipango  na Mthamini  daraja la pili mapema wiki hii, baada ya kughushi nyaraka ili kujipatia fedha za malipo ya pango.

  Bw. Haonga alipokea fedha za malipo ya pango kiasi cha shilingi milioni saba kutoka kiwanda cha OLAM Tanzania mwezi Juni mwaka huu.

  Akizungumza kwa njia ya simu,  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda, Mkoa wa Mara, Bi. Janeth Mayanja alisema kuwa Bw. Haonga amekiuka Sheria za Utumishi wa Umma, kanuni ya 42 na uamuzi uliotolewa na baraza la madiwani  ni sahihi.

  Bi. Janeth alisema “Bw. Eliud Haonga alihifadhi shilingi milioni mbili tu katika akaunti ya Halmashauri ya Mji wa Bunda  na kutumia shilingi milioni tano kwa matumizi yake binafsi”.“Maamuzi haya yamechukuliwa baada ya Kamati ya Uchunguzi  kumaliza kazi yake kwa mujibu wa  Sheria, kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma.” alisema  Bi. Mayanja.

  Aidha,  Bi. Mayanja amewaasa watumishi wa Halmashauri  Bunda  kujiepusha na vitendo vinavyoashiria wizi na ubadhirifu,  na hatua kali  zitachukuliwa kwa yeyote atakayekiuka maadili ya utumishi wa umma.
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda, mkoa wa Mara Bi. Janeth
  Mayanja akiwa Ofisini kwake.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Baraza la Madiwani Lamfukuza Kazi Mtumishi. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top