728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, November 9, 2016

  Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania ametembelea shule za msingi Mjini Dodoma kuona utekelezaji wa Mpango wa Kuinua ubora wa elimu Nchini unaotekelezwa na Wizara ya Elimu chini ya ufadhili wa Serikali ya Uingereza


  Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania, Sarah Cooke akisikiliza maelezo kutoka kwa Mratibu Elimu Kata ya Msalato Ally Swalehe juu ya mfumo wa taarifa shuleni, ambapo mpango umetoa tablet kwa walimu wakuu na waratibu elimu kata. Kushoto kwake ni afisa elimu Mkoa wa Dodoma, Maria Lyimo.

  Wanafunzi wa Shule ya Msingi Msalato wakiimba wimbo wa kumkaribisha Balozi wa Uingereza Nchini alipotembelea shule hiyo. 

  Wanakijiji wa Chihanga ambao walihamasika na programu ya kuinua ubora wa elimu Nchini na kuanzisha kituo cha utayari kwa watoto wao ambao walikuwa wanashindwa kwenda kwenye shule mama kutokana na umbali, wakicheza ngoma ya kigogo kumkaribisha Balozi.
  Balozi Sarah Cooke akiwa na watoto wa kituo cha utayari cha Chihanga ambapo kabla ya hapo watoto hao walikuwa nyumbani , uwepo wa kituo hicho umewawezesha watoto kufurahia michezo mbali mbali kama vile kuimba na kujifunza maneno ya Kiswahili ili wawe tayari kwa kuanza darasa la kwanza. Kituo kilianzishwa mwaka jana na hii ni awamu ya pili ambayo ina jumla ya watoto 64 

  Balozi akifurahia jambo na Afisa Elimu wa mkoa wa Dodoma, Maria Lyimo

  Baadhi ya zana za kujifunzia watoto katika kituo cha utayari Chihanga

  Balozi akikaribishwa katika kituoa cha utayari Chihanga

  Watoto wa kituo cha utayari wakiwa wamejiandaa kumuimbia balozi baadhi ya nyimbo wanazojifunza kituoni.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania ametembelea shule za msingi Mjini Dodoma kuona utekelezaji wa Mpango wa Kuinua ubora wa elimu Nchini unaotekelezwa na Wizara ya Elimu chini ya ufadhili wa Serikali ya Uingereza Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top