728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, November 15, 2016

  BALOZI WA INDIA NCHINI AMTEMBELEA WAZIRI WA MAMBO YA KATIBA NA SHERIA DKT HARRISON MWAKYEMBE

  Balozi wa INDIA nchini Mh. Sandeep Arya amemtembelea Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe ofisini kwake jijini Dar es salaam na kuzungumza jinsi kuiendeleza sekta ya Sheria nchini na kuimarisha uhusiano uliopo baina ya Tanzania na India kupitia sekta hiyo.

  Akizungumza walipokutana katika kikao hicho Mhe. Waziri Dkt Mwakyembe ameelezea kufurahishwa kwake na uhusiano uliopo baina ya nchi hizo na kuelezea haja yake yake ya kuiomba INDIA kuangalia namna inavyoweza kuwajengea uwezo wataalamu wa sheria nchini ili kupata wataalamu bora zaidi wa sheria ambao wataisaidia nchi kusonga mbele.

  Alisema INDIA imekuwa na uzoefu wa muda mrefu katika eneo la sheria na anaona litakuwa jambo bora kwa nchi hiyo kuendesha zoezi la kubadilishana wataalamu katika sekta hiyo ili kuwapatia ujuzi na utaalamu zaidi wataalamu wa Tanzania ambao ndio kwanza wanachipukia katika aneo hilo.

  Amesema uanzishwaji wa vyuo vikuu vingi vinavyofundisha sheria nchini pia umeleta changamoto ya aina yake kwa nchi na kuongeza kitendo cha kusaidia katika eneo hilo kutasaidia kutatua changamoto hiyo na kukuza na kuimarisha sekta hiyo nchini.

  Naye Mhe. Balozi Arya alielezea utayari wa nchi yake kuisaidia Tanzania katika eneo hilo na kusema kwamba iko tayari kusaidia harakati za kukuza na kuimarisha sekta ya sheria nchini. Alisema India imekuwa ikitoa nafasi za mafunzo ya muda mrefu na mfupi katika fani mbalimbali na kuongeza kuwa sasa inaangalia kuongeza sekta ya Sheria katika miongoni mwa maeneo ya ya kipaumbele na hivyo kuwapatia ujuzi na utaalamu wataalamu wa fani hiyo nchini kwa kuwapatia nafasi za kujifunza nchini India.
  Balozi wa India nchini Tanzania Mh. Sandeep Arya akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe alipomtembelea ofisini kwake leo (15/11/2016) jijini Dar Es Salaam.
  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe akijadiliana jambo na mgeni wake Balozi wa India nchini Tanzania Mh. Sandeep Arya alipomtembelea ofisini kwake leo (15/11/2016) jijini Dar Es Salaam.
  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa India nchini Tanzania Mh. Sandeep Arya mara baada ya kumaliza mazungumzo yao leo (15/11/2016) jijini Dar Es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: BALOZI WA INDIA NCHINI AMTEMBELEA WAZIRI WA MAMBO YA KATIBA NA SHERIA DKT HARRISON MWAKYEMBE Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top