728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, November 9, 2016

  ATI KUTUMIA DOLA ZA KIMAREKANI BILIONI 1.2 KUIMARISHA SEKTA YA NISHATI

  Wakala wa Bima ya Biashara Afrika (ATI) umeitaka serikali ya Tanzania kuimarisha ushirikiano uliopo baina yake ili kuwekeza dola za Marekani bilioni 1.2 (2.6tr/-) katika sekta ya nishati utakaoongeza megawati 1,200 katika gridi ya taifa. 
   
  Tanzania ni mmoja wa wajumbe waliasisi ATI wakala ambao ulianzishwa ili kutoa bima kwa wawekezaji pamoja na kufanya shughuli nyingine za kibiashara miongoni mwa nchi za Afrika ambazo ni wanachama. Chini ya ubia ambao ulisainiwa na Rais Mstaafu Mheshimiwa Benjamini William Mkapa mwaka 2001, Tanzania na nchi nyingine zilikubaliana kutoa upendeleo wa kupata mkopo katika miradi yote inayoungwea mkono na ATI. 
   
  Ahadi hiyo ambayo inatoa uhakika kwa nchi mwanachama ambao utaiepusha na madai yoyote katika miradi inayoungwa mkono na ATI, kuwapatia wawekezaji, wagavi na na nafasi nyingine muhimu katika kuzindua miradi Tanzania. 
   
  “Lengo letu ni kuisaidia Tanzania kwa kuuleta nchini uwekezaji unaohitajika sana na kupunguza gharama za kukopa. Sisi ni watu wakimya lakini ni sehemu muhimu sana ya fumbo kwa sababu tumesimama nyuma ya uwekezaji na biashara ambayo inakadiriwa kufikia dola bilioni (2tr/-) nchini Tanzania tangu kuanza kwa biashara mwaka 2004”, alibainisha Ofisa Mtendaji Mkuu wa ATI George Otieno. Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Bima ya Biashara Afrika (ATI) George Otieno akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) wakati wa mkutano maalum uliofanyika Jijini Dar es salaam kwa lengo la kuwaeleza wanatazania juu ya kinachojadiliwa katika mkutano wa jukwaa la kimataifa la sekta ya nishati ambalo likiwa na kauli “Kufungua uwekezaji kutawezesha ongezeko kubwa la Nishati Tanzania” ambalo limeitishwa na ATI mkutano ambao unafanyika Jijini Dar es salaam. Tusekile Kibonde ambaye ni Underwriter Responsible for Tanzania Kutoka ATI akieleza maswala mbalimbali mbele ya wanahabari juu ya Mkutano huo ambao unafanyika Jijini Dar es salaam ambapo Jukwaa hilo linawakutanisha pamoja wadau kutoka Nyanja binafasi za umma katika kutafuta masuluhisho ambayo yataondoa hatari zinazoikabili sekta ya nishati ili kuvutia uwekezaji unaohitajika sana.
  Kamishna msaidizi wa Umeme wa wizara, mhandisi Innocent Luoga akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) wakati wa mkutano maalum uliofanyika Jijini Dar es salaam kwa lengo la kuwaeleza wanatazania juu ya kinachojadiliwa katika mkutano wa jukwaa la kimataifa la sekta ya nishati ambalo likiwa na kauli “Kufungua uwekezaji kutawezesha ongezeko kubwa la Nishati Tanzania” ambalo limeitishwa na ATI mkutano ambao unafanyika Jijini Dar es Salaam.
  Viongozi wakiwa katika picha ya pamoja. Tanzania inaweza kunufaika zaidi kutokana na ubia wake na ATI kirahisi kwa kurudia utekelezaji wa ahadi zake kwa kusaidia miradi inayoungwa mkono na ATI ndani ya Tanzania. Chini ya masharti ya ubia, Tanzania inaweza kuwepo kiwango mbadala wa vipimo vya viwango kwa kipimo cha uwekezaji cha ATI daraja A mara tutakaposaini manunuzi yanayoungwa mkono na ATI.
   
  Chini ya kanuni za Basel, ambazo zinasimamia mabenki mengi ya kimataifa, ynaweza kuikopesha nchi kama Tanzania ikiwa inaungwa mkono katika bima na taasisi kama ATI, ambayo ni taasisi inayoheshimika na inayoaminiwa na masoko ya kimataifa ya fedha. Bima ya ATI inaiwezesha benki kupunguza kiwango cha mwisho cha malipo ya bima, ambacho kwa kiwango kikubwa kinapunguza gharama za kukopa kwa Tanznaia na nchi nyingine za Afrika ambazo ni wanachama. 
   
  Kushindwa kutumia kikamilifu fursa hii, Tanzania inaweza kukosa uwekeza wenye thamani ya mamilioni ya fedha. “ATI inaweza kuisaidia nchi kuwa inavutia kuwekeza kifedha kwa kuvutia uwekezaji zaidi. Hili ni muhimu hususani katika sekta ya nishati ambayo kwa hivi sasa ina ushindani mkubwa,” alisema Mdhamini Mkazi wa ATI nchini Tanzania Tusekile Kibonde.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: ATI KUTUMIA DOLA ZA KIMAREKANI BILIONI 1.2 KUIMARISHA SEKTA YA NISHATI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top