Na.
Immaculate Makilika, MAELEZO
Serikali
imesema kuwa ziara ya Mfalme wa Morocco nchini Mohammed wa VI ina lengo la kukuza diplomasia ya uchumi kati ya nchi
hizi mbili, na kamwe haitaathiri msimamo
wa Tanzania katika mgogoro unaoendelea kati ya Morroco na Sahara Magharibi.
Hayo
yameelezwa katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, ambapo taarifa hiyo imesisitiza kuwa ziara hiyo itakuza ushirikiano
katika masuala ya uchumi.
“
Lengo la ziara hiyo ni kukuza zaidi uhusiano kati ya Tanzania na Morocco
hususani katika masuala ya kiuchumi na kibiashara kwa faida ya watu wa nchi
hizi mbili, na kamwe haitaathiri msimamo
wa Tanzania katika mgogoro unaoendelea kati ya Morocco na Sahara Magharibi”.
Hata
hivyo taarifa hiyo imesisitiza kuwa , msimamo wa Tanzania ambao umekuwa ukisimamiwa
na Awamu zote za uongozi zilizopita na Awamu
hii, upo sambamba na ule wa Umoja wa Afrika (AU) unaoutaka Umoja wa Mataifa (UN)
ambao ndio wamepewa jukumu la kusimamia mgogoro huo, kuongeza kasi ya kutatua
mgogoro huo ili kupata suluhu ya kudumu.
Mfalme
Mohammed wa VI wa Morocco anatarajiwa kuwasili nchini Oktoba 19 mwaka huu kwa
ziara ya siku nne, ambapo atatembelea Zanzibar pamoja na Hifadhi ya Ngorongoro
kwa ajli ya kujionea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.
Aidha,
mara baada ya kumaliza ziara yake nchini, Mfalme Mohammed VI atatembelea nchi
za Rwanda, Ethiopia na Kenya.
0 comments:
Post a Comment