728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Sunday, October 9, 2016

  WAZEE WASTAAFU WANAWEZA KUWA MABILIONEA NA KUIBADILISHA NCHI

  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni (PSPF) Adam Mayingu, akizungumza na wanachama wa Chama Cha Walimu Wastaafu jiji la Tanga (Chajiwata) wakati wa maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Mteja jana. kulia anaemwangalia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella.

  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni (PSPF) Adam Mayingu, akipokea Hati na Katiba ya Chama Cha Walimu Wastaafu jiji la Tanga (Chajiwata) kutoka kwa aliekuwa Afisa Elimu shule ya Msingi jiji la Tanga, Damass Kifanga.  Wanachama wa Chama Cha Walimu Wastaafu jiji la Tanga (Chawajita) , wakifuatilia hotuba ya mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Pensheni (PSPF), Adam Mainga, wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja kwa walimu wastaafu uliofanyika Tanga jana.  Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella, akifungua mkutano wa wanachama wa Chama Cha Walimu Wastaafu jiji la Tanga, (Chawajita) wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja wa Mfuko wa Pensheni (PSPF) uliofanyika Tanga  Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu Wastaafu jiji la Tanga, (Chajiwata) Debora Daffa, akizungumza katika mkutano wa Mfuko wa Pensheni (PSPF) wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja mkutano uliofanyika Tanga jana.  Mwanachama wa Chama Cha Walimu Wastaafu jiji la Tanga (Chajiwata) Roda Matoi, akizungumza katika mkutano wa Mfuko wa Pensheni (PSPF) na walimu wastaafu wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja na kufanyika ukumbi wa mikutano jengo la Mkuu wa Mkoa wa Tanga jana
  Viongozi wa Chama Cha Walimu Wastaafu jiji la Tanga (Chajiwata) pamoja na STAFF ya Mfuko wa Pensheni (PSPF) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella mara baada ya mkutano na walimu wastaafu wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja mkutano uliofanyika jana ukumbi wa mikutano jengo la Mkuu wa Mkoa. Blog ya kijamii Tangakumekuchablog 0655 902929


  ……………………………………………………………………
  MKURUGENZI wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF hapa nchini, Adam Mayingu amesema kuwa wazee wastaafu wanauwezo wa kuwa mabilionea na kuibadilisha nchi kwa kutengeneza ajira ,kubuni miradi inayoweza kuwaingizia kipato baada ya kulitumikia taifa katika nafasi mbalimbali walizokuwa nazo.

  Alisema kwani asilimia kubwa wanaweza kuanzisha miradi mbalimbali ambayo inaweza kuwasaidia kujiongezea kipato hali itakayopelekea vijana kuweza kuinua maisha yao kitendo ambacho pia kitasaidia kuongeza pato la serikali.

  Mayingu aliyasema hayo wakati wa wiki ya huduma kwa wateja Duniani ambapo mfuko huo unakutana na wadau wake ili kuweza kubaini changamoto ambazo ikiwemo kuangalia namna ya
  kukabiliana nazo.

  Wiki hiyo ilikwenda sambamba na uzinduzi wa chama cha wazee wastaafu wilayani Lushoto (Chawisewilu) chenye makazi yake mjini hapa waliokuwa wakifanya kazi na baadae kustaafu waliweza kuhudhuriwa kwa wingi na kutoa mapendekezo yao.


  “Ukiangalia wazee wastaafu wanapokuwa wamepata fedha zao za kiunua mgongo badala ya kwenda kuzitumia katika matumizi yasiyokuwa ya lazima badala yake waone namna ya kuzitumia kubuni miradi itakayokuwa chachu kwao kupitia hatua kubwa za kimaendeleo “Alisema.

  “Sisi kama Mfuko wa Pensheni wa PSPF tunaunga mkono chama chenu lakini pia niwaambie Sido wapo tuzungumze nao ikiwemo kuweka utaratibu mzuri ili muweza kuona namna ya kuweza kunufaika na uwepo wao “Alisema.

  “Lakini pia msisite kuwatumia wataalamu kwenye masuala mbalimbali ya ujasiriamali kwani hiyo ndio njia ambayo inaweza kuwa chachu ya kuweza kufikia malengo yenu hasa katika kipindi hiki kwa kushirikiana “Alisema.

  Aidha pia aliwataka kupitia umoja wao kutumia fursa nyingi zilizopo kwenye maeneo yao kwani wanao umri wa kuishi mkubwa badala yake yaondokana na dhani ya kuwa watu wanapokuwa wakistaafu wanafariki kitendo ambacho sio hakina ukweli wowote.

  Lakini pia aliwataka kutumia fursa hiyo waliyoipata kuieli misha jamii huku akiwaomba kupitia chama chao kuwahimiza vijana wao kujiunga ma mfuko wa Pensheni wa PSPF ili waweze kunufaika na mafao yanayotolewa.

  Awali akizungumza wakati akifungua kikao hicho,Kaimu Mkuu wa wilaya ya Lushoto,Asha Kikoti aliwataka wazee wastafu kuhakikisha fedha wanazozipata za kiunua mgongo kuweka mpango mzuri wa kuzitumi kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo ili waweze kujiingizia
  kipato.

  “Kiuhalisia wazee wastaafu wanapopata fedha zao wanaona kama vile ni
  nyingi na kuzitumia bila kwa haraka bila kufikiria hata kuzianzishia miradi
  ambayo inaweza kuwasaidia kupambana na ukali wa maisha “Alisema huku
  akiwasisitizia wabadilike.

  Sambamba na hayo aliwataka pia kuwa na mpango mzuri wa matumizi ya fedha zao za kiinua mgongo ili ziweze kuwasaidia kutumiza ndoto zao katika maisha ikiwemo kuwa na maisha
  mazuri.

  Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: WAZEE WASTAAFU WANAWEZA KUWA MABILIONEA NA KUIBADILISHA NCHI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top