728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, October 25, 2016

  WATANZANIA WAASWA KUTUMIA BIDHAA ZINAZOZALISHWA NA VIWANDA VYA NDANI-MWIJAGE

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, imesema kulinda viwanda vya ndani ni lazima watanzania wanunue bidhaa zinazozalishwa ndani na kuacha bidhaa zinazozalishwa nje ya nchi.

  Hayo ameyasema leo, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, wakati akitangaza maonesho ya viwanda vya ndani yatakayofanyika Desemba 7 hadi 11 katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.

  Mwijage amesema nchi zilizofanikiwa kwa viwanda imetokana na watu wao kupenda kununua bidhaa zao ambapo na Tanzania inatakiwa kufanya hivyo kwa wananchi kupenda bidhaa zao

  Amesema viwanda vya ndani katika kuweza kuzalisha bidhaa na zikaweza kutoka ni lazima wazalishe bidhaa zenye ubora kwa kupata soko la ndani na nje ya nchi. ‘’Kauli mbiu ya maonesho hayo ni Tanzania sasa tunajenga viwanda ambapo kila mtu anaweza kuanzisha kiwanda chake na kuzalisha na kuweza kupata soko la uhakika’’.

  Amesema maonesho hayo yatakutanisha wadau mbalimbali wa viwanda ambapo watanzania wenye nia kuanzisha viwanda watumie maonesho hayo kuweza kupata mwongozo kutoka kwa wataalam jinsi ya kuanzisha kiwanda. Aidha amesema katika maonesho hayo kwa wanafunzi waliohitimu katika vyuo watumie fursa katika ya kutafuta ajira kwa viwanda vitavyoshiriki maonesho hayo.

  Amesema Wakuu wa Mikoa wote wataalikwa kuweka maeneo yao waliopanga kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda ikiwa ni pamoja kuondoa masharti magumu kwa wawekezaji wanakwenda kuomba ardhi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: WATANZANIA WAASWA KUTUMIA BIDHAA ZINAZOZALISHWA NA VIWANDA VYA NDANI-MWIJAGE Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top