728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, October 13, 2016

  Wasomi kutembelea Nyumba ya Mwalimu Nyerere Magomeni Kesho


  Mratibu wa ziara ya viongozi wa vyuo vikuu mkoa wa Dar es Salaam,Marco Bujiba ,akizungumza na waandishi wa wahabari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam,kulia mratibu msaidizi Boniface Macheta.

  Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii

  Umoja wa wanafunzi wa elimu ya juu kutoka vyuo mbalimbali wamejipanga kuadhimisha siku ya Nyerere Day kwa kutembelea nyumba ya kihistoria aliyowahi kuishi mwalimu Nyerere iliyopo Magomeni jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mratibu wa safari hiyo Rais wa Chuo cha Sayansi na tiba Muhimbili,Marco Bujiba amesema kuwa wameamua kufanya hivi hilinkupata muda wa kutafakari kwa upana juhudi za baba wa Taifa katika kulikomboa Taifa dhidi ya Wakoloni kupambana na umaskini ,Ujinga na maradhi ambavyo alivitaja kama maadui wakubwa wa Taifa letu pamoja na kupinga vita rushwa ,ubaguzi miongoni miongoni mwa watanzania kwa tofauti za makabila ,dini,rangi au maeneo yanayotoka.

  "Kama viongozi vijana katika nchi yetu ,tutatumia fursa hiyo kutathimini hatua za kimaenedeleo tulizifanya kama taifa kwa kurejea mpango wa Taifa wa kuondoa umaskini na kukuza Uchumi ili kujua kwa kwa kiasi gani taifa letu limeenzi fikra za Mwalimu kwa vitendo katika kupambana na adui namba moja wa Tanzania ,yaani umaskini" amesema Marco.

  Aliongeza kuwa kwa kufanya hivi itaongeza chachu ya kujituma kujenga taifa namkusaidia kuhamasisha vijana wote Tanzania kwa kufanya kazi kwa bidii ili kuondoa umaskini hivyo kutimiza kwa vitendo kauli mbiu ya Serikali ya Hapa Kazi.

  Pia alitumia fursa hiyo kuwaomba viongozi wote ambao ni viajna kuenzi fikra za baba wa taifa katika kulitumikia taifa .
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Wasomi kutembelea Nyumba ya Mwalimu Nyerere Magomeni Kesho Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top