728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, October 31, 2016

  Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wapongeza Muswada Habari


  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Dodoma

  Baadhi ya Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini (GCU) wamemesema Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa mwaka 2016 ni muhimu kwa taifa na unalenga kuleta tija kwa taifa zima.

  Muswada huo unalenga kuwanufaisha waandishi wa habari, wamiliki wa vyombo vya habari pamoja na wananchi wa kawaida nchini.

  Wakipongea kwa nyakati tofauti na mwandishi wa habari hii, Wakuu hao leo wa wamesema muswada huo una manufaa na fursa nyingi kwa taifa na wananchi tofauti na hali ilivyokuwa hapo awali.

  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Zawadi Msalla amesema kuwa sheria hiyo inatoa mwanya mkubwa kwa tasnia ya habari nchini kuwa ni miongoni mwa taaluma inayoheshimika kama kada nyingine kwa kuwa na chombo kitakachowasimamia wanahabari hao.

  “Uanzishwaji wa Baraza Huru la Habari ni moja ya takwa lililowekwa na Sera ya habari na Utangazaji ya mwaka 2003 iliyoitaka Serikali kuanzisha chombo huru kitakachosimamia masuala ya habari hivyo,muswada huu utakapokuwa sheria utakuwa umetekeleza agizo la Serikali la kuanzisha chombo huru kitakachosimamia masuala ya habari”, alisema Msalla.

  Zawadi ameongeza kuwa kuanzishwa kwa Sheria hiyo itasaidia kuleta uhuru wa vyombo vya habari na wanahabari kufanya kazi yao ipasavyo kwani kwa sasa mmiliki wa chombo cha habari asiporidhishwa na maamuzi ya kutopewa leseni anakata rufaa kwa Waziri mwenye dhamana na asiporidhishwa na maamuzi yaliyotolewa na Waziri huyo amepewa fursa ya kwenda mahakamani.

  Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Mkoa wa Morogoro, Andrew Chimesela amepongeza juhudi za Serikali kwa kazi ya kuandaa Muswada ambao utasaidia kuwa na Sheria itawanufaisha wadau wote wa habari nchini.

  Baada ya kupitishwa Muswada na Bunge, kuidhinishwa na kusainiwa na Rais hatimaye kuwa Sheria, Chimesela kuwa ziandaliwe kanuni ambazo zinaendana na wakati huu wa sasa tofauti na ilivyokuwa wakati wa Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976.

  Aidha, amekubaliana na uamuzi wa kuundwa kwa Bodi ya Ithibati kwa sababu bodi hiyo itakua na kazi ya kuangalia maslahi ya wanatasnia pamoja na kudhibiti nidhamu na maadili ambayo yanapaswa kwenda sambamba na tasnia habari ili iweze kuheshimika kama taaluma nyingine za Wanasheria, wahasibu na sekta ya afya.

  Naye Mkuu wa Kitengo cha GCU kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Englibert Kayombo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), wameunga mkono uanzishwaji wa Bodi ya Ithibati kwasababu itasaidia kutambua wanahabari wenye taaluma halali kwenye sekta ya habari nchini.

  “Binafsi naunga mkono jitihada zinazofanywa na Wizara za kurasimisha tasnia hii ya habari ili iwe na hadhi sawa na tasnia zingine, ni vyema kuratibu kazi za waandishi wa habari ili waweze kutoa habari zenye kujenga taifa letu imara lenye mfumo mzuri wa kazi za kihabari”, alisema Kayombo.

  Baada ya kuanzishwa na kufanya kazi Sheria hiyo, ni dhahiri itavifanya vyombo vya habari nchini kuajiri watu wenye taaluma ya habari tofauti na hali ilivyosasa na wananchi watarajie kupata habari za ukweli na uhakika.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wapongeza Muswada Habari Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top