728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, October 3, 2016

  Waandaaji wa miswada ya filamu nchini watakiwa kuzingatia maadili ya kitanzania.

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akifunua pazia kwa ajili ya kuzindua Nembo ya Bodi ya Filamu pamoja na shindano la uandishi bora wa miswada ya filamu wakati wa kikao cha kupitia uchambuzi wa hali ya Tasnia ya Filamu Tanzania kwa ajili ya ukamilishaji wa sera ya filamu na namna ya kuboresha filamu za ndani leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Bw. Silvester Sengerema na katikati ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo.

  Katibu Mkuu Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Bw. Methew Biko (kushoto aliyesimama) akitoa salamu za shirikisho hilo kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) wakati wa kikao cha kupitia uchambuzi wa hali ya Tasnia ya Filamu Tanzania kwa ajili ya ukamilishaji wa sera ya filamu na namna ya kuboresha filamu za ndani leo Jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo.
  Mtendaji Mkuu TaSUBa Dkt. Herbart Makoye akizungumza na wadau wa filamu (hawapo pichani) walioshiriki katika kikao cha kupitia uchambuzi wa hali ya Tasnia ya Filamu Tanzania kwa ajili ya ukamilishaji wa sera ya filamu na namna ya kuboresha filamu za ndani leo Jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo (kushoto) akifafanua jambo wakati wa kikao cha kupitia uchambuzi wa hali ya Tasnia ya Filamu Tanzania kwa ajili ya ukamilishaji wa sera ya filamu na namna ya kuboresha filamu za ndani leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Bw. Silvester Sengerema.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na wadau wa filamu (hawapo pichani) walioshiriki katika kikao cha kupitia uchambuzi wa hali ya Tasnia ya Filamu Tanzania kwa ajili ya ukamilishaji wa sera ya filamu na namna ya kuboresha filamu za ndani leo Jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wadau wa filamu wakifuatilia kwa makini mada zilizokua zikitolewa wakati wa kikao cha kupitia uchambuzi wa hali ya Tasnia ya Filamu Tanzania kwa ajili ya ukamilishaji wa sera ya filamu na namna ya kuboresha filamu za ndani leo Jijini Dar es Salaam.  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (watano kulia) katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa filamu walioshiriki katika kikao cha kupitia uchambuzi wa hali ya Tasnia ya Filamu Tanzania kwa ajili ya ukamilishaji wa sera ya filamu na namna ya kuboresha filamu za ndani leo Jijini Dar es Salaam. Wane kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo na wasita kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Bw. Silvester Sengerema.

  Picha na: Genofeva Matemu na Raymond Mushumbusi WHUSM

  ……………………………………………………

  Na Genofeva Matemu na Raymond Mushumbusi.

  Waandaaji wa miswada ya filamu nchini wametakiwa kuhakikisha kwamba maudhui ya miswada inayoandaliwa inazingatia maadili na utamaduni wa Kitanzania ili kuifanya sera shirikishi inayoandaliwa kuwa na tija.

  Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokua akifungua kikao cha Wadau wa Filamu kupitia uchambuzi wa hali ya Tasnia ya Filamu Tanzania kwa ajili ya ukamilishaji wa sera ya filamu na namna ya kuboresha filamu za ndani leo Jijini Dar es Salaam.

  “Maudhui ya miswada ya filamu ikiandaliwa kwa kuzingatia maadili ya kitanzania itaboresha tamaduni zetu na kuzifanya kazi za sekta ya filamu kufanywa kwa kuzingatia weledi hivyo kuiona tasnia kama chombo kimojawapo kinachoisaidia Serikali sio tu kutoa burudani bali pia elimu kwa wananchi” amesema Mhe. Nnauye.

  Aidha Mhe. Nnauye amesema kuwa mapinduzi ya sekta ya filamu hapa nchini yanawezekana iwapo kazi zake zitaonekana katika kiwango cha ubora kwa kuangalia maudhui yaliyomo na mapokeo yake kwa jamii.

  “Napenda kuona wasanii wetu wanakuwa wabunifu badala ya kuwa na filamu zenye maudhui ya aina moja kwa kuzingatia weledi na kuendana na maendeleo ya sayansi na teknolojia ili kuweza kukidhi masoko ya filamu nje ya nchi” amesema Mhe. Nnauye.

  Naye Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo amesema kuwa kutokana na kukua kwa Tasnia ya Filamu kuna uhitaji wa Sera ya Filamu ili iweze kuwa dira ama mwelekeo na mwongozo katika kukuza tasnia hii na kuwezesha kuongezeka kwa fursa za uwekezaji, motisha na fursa za mitaji katika tasnia ya filamu nchini.

  Bibi Fissoo amesema kuwa kukamilika kwa Sera ya Filamu kutabadidlisha kabisa taswira nzima ya Sekta ya Filamu hapa nchini kwani itaboresha uzalishaji wa bidhaa bora zenye kuzingatia weledi, filamu kuangaliwa kama chombo cha kukuza uchumi kwa manufaa ya Taifa na watanzania wote.

  Kwa upande wake Katibu Mkuu Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Bw. Methew Biko ameishukuru serikali kupitia Bodi ya Filamu na Idara ya Sera na Mipango kwa kusikia kilio cha muda mrefu cha wanatasnia wa filamu kuhitaji Sera ya Filamu na kuahidi ushirikiano wa dhati kutoka kwa wadau wa filamu ili kufanikisha uandaaji ya sera hiyo.

  Kikao cha kupitia uchambuzi wa hali ya Tasnia ya Filamu Tanzania kimehusisha Wakurugenzi wa Idara, Wakuu wa Taasisi za Serikali na binafsi, wadau mbalimbali wa Tasnia ya Filamu wakiwemo wanazuoni, waigizaji, watayarishaji, waongozaji wa filamu, waandishi wa miswada, pamoja na wawekezaji.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Waandaaji wa miswada ya filamu nchini watakiwa kuzingatia maadili ya kitanzania. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top