728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, October 11, 2016

  VITENDO VYA USHOGA NI KOSA LA JINAI NA HATUA KALI ZITACHUKULIWA KWA WANAOHAMASISHA VITENDO HIVYO

  Serikali haitavumilia watu au taasisi yoyote watakaobainika kuhusika na uhamasishaji wa vitendo vya ndoa za jinsia moja nchini kwa kuwa vitendo hivyo ni kosa la jinai  na kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtu, kikundi au taasisi itakayobainika kufanya uhamasishaji, kuficha na kuendesha vitendo hivyo nchini
  .
  Waziri wa Mambo  ya Katiba na Sheria amesema hayo mjini Dar es salaam leo alipokutana na waandishi wa habari kuelezea kauli iliyotolewa na Serikali ya Marekani kuwa Tanzania inakiuka haki za binadamu kwa kutowatambua na kuwabagua katika kuwapatia huduma za afya wale walioathirika na ukimwi, kifua kikuu na vvu watu wanaojihusisha na ndoa za jinsia moja nchini. 

  Amesema Tanzania haina na haijawahi kuwa na Sheria, Sera, kanuni au muongozo ambao unalenga kuwabagua waathirika wa ukimwi, vvu na kifua kikuu na kuongeza kuwa waathirika wote wanapata huduma zote stahili  bila ya kuulizwa au kujali kuwa wamepatajepataje maambukizi ya maradhi hayo kama ambavyo sera ya Afya inavyosema .Amesema Serikali ya Awamu ya Tano haiko tayari kuendeshwa huku ikiangalia sheria za nchi zikivunjwa kupitia vitendo visivyo vya kimaadili na hatimaye kuiletea nchi madhara makubwa kwa wakati huu na kwa baadae.

  "Serikali hii haiko tayari kuendeshwa endeshwa bila ya kuwa na principles na mambo ya kihovyo kama hayo hayawezi kuachwa yakiendelea , hayatavumiliwa au kufumbiwa macho kwa migongo ya kupata misaada ya kifedha kutoka kwa nchi zilizoendelea au mashirikia makubwa ya Kimataifa namna hiyo "

  Amesema Serikali haitalala na itaionyesha dunia kuwa nchi hii kuna utawala wa sheria na hakuna mambo ya hovyo yatakayoachwa yafanyike kila wanavyotaka kupitia miamvuli ya kutoa misaada kwa nchi hii hasa kisingizio cha kupambana na virusi vya ukimwi, na  Ukimwi.

  Amesema Serikali inayo uishahidi kuwa kuna Asasi 15 nchini yenye uhusiano na nchi zilizoendelea  ambayo yanajihusisha na uhamasishaji wa vitendo vya ndoa za jinsia moja kwa mwamvuli wa kusaidia harakati dhidi ya magonjwa ya kifua kikuu, ukimwi na vvu.

  Amesema serikali imefuatilia kwa undani suala hilo na kugundua kuwa asasi hizo zimejikita na kuendesha uhamasihaji katika mikoa 11 nchini ambayo ameitaja kuwa ni Dar es salaam, Arusha, Shinyanga, Mbeya, Iringa, Tabora, Dodoma, Kilimanjaro, Njombe, Lindi na Morogoro.Amesema ushahidi uliopo unaonyesha kuwa asasi hizo zimekuwa zikifanya mikutano  ya siri na sherehe  usiku, kuandaaa na kuchapisha machapisho yanayohamasisha vitendo hivyo , kusambaza vilainishi na kondom na kupeleka elimu ya ushoga katika shule za msingi na sekondari nchini.

  Amesema hayo yote yamekuwa yakifanyika kupitia mwamvuli wa kutoa misaada ya kusaida waathirika wa Ukimwi na VVU wkati wakijua kuwa hayo wanayoyafanya yana ajenda nyingine ambayo haitoa afua kwa magonjwa hayo kama wanavyosema.Amesema kuwa serikali imegundua kuwa Tanzania imepangwa kuwa kitovu cha vitendo hivyo katika ukanda wa nchi za Kusini mwa Afrika na Afrika Mashariki.

  Amesema kutokana na mpango huo Serikali iko tayari kukosa hiyo misaada ili kuifanya Tanzania kuwa nchi salama kwa sasa na kwa kizazi kijacho huku ikizingatia mila, tamaduni, desturi na imani za kidini kama ilivyokuwa tangu zama na zama.Mhe. Waziri Dkt Mwakyembe amemtaka Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome kukutana na Makatibu wakuu wenzake kutoka Wizara za Afya, Mambo ya Ndani na Viwanda na Biashara ili kutafakari ni wapi kama nchini ilikosea hadi kujikuta katika hali na kuangalia cha kufaanya ili kujikwamua katika hali hii na kuchukua hatua kali za ksiheria kwa taasisi ambazo zinajihusisha na uhamsishaji wa vitendo hivyo nchini.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: VITENDO VYA USHOGA NI KOSA LA JINAI NA HATUA KALI ZITACHUKULIWA KWA WANAOHAMASISHA VITENDO HIVYO Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top