728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, October 31, 2016

  UWEPO WA BARAZA HURU LA HABARI UTASAIDIA KUKUZA MAADILI KWA WANAHABARI.


  Na Daudi Manongi.

  UWEPO wa kifungu kinachopendekeza uanzishwaji wa Baraza Huru la Habari katika Muswada wa Huduma ya Habari wa mwaka 2016 utasaidia kukuza maadili na viwango vya taaluma baina ya wanahabari na Kampuni za habari nchini.

  Maoni hayo yametolewa na Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Dk Jim James Yonazi leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hizi

  Ameongeza kuwa chombo hicho ni umuhimu kusimamia maadili ya Taalum ya habari na kufanya waandishi wa habari hapa nchini wawajibike kwa kazi zao za kila siku za kuhabarisha umma. Mhariri huyo Mtendaji amewahasa wanahabari kuukubali muswada unaopendekezwa kwani ni kwa maslahi yao wenyewe na utaipa heshima taaluma hii.

  “Sheria hii ni muhimu sana kwa kuwa ukiangalia katika sekta zingine kama za Uhasibu, Uhandisi ,wakandarasi na wanasheria wanatambuana kupitia vyombo ambavyo wamejiwekea wakati sekta ya Habari hakuna kitu kama hicho kinachoweza kuonyesha huyu ni mwanahabari na hata kufahamu idadi yao nchini ni ngumu hata kuiendeleza katika viwango vya juu uwezekano huo haupo”alisema Dk Yonazi.

  Aidha amewataka wamiliki na wadau wa tasnia ya Habari kuangalia mapungufu yake na kuona ni wapi panatakiwa kuboreshwa na kusisitiza ni vema kuwa na sheria hii kwanza halafu mapungufu yatafanyiwa kazi baadaye.

  Kwa upande mwingine amewataka wandishi kutokuwa waoga wa muswada huu na kutoa maoni yao kama wafanyavyo katika mambo mengine na kuwataka kwa sasa kuruhusu utekelezaji wa muswada huu na kuendelea kuusimamia na kuufatilia ili kujua wapi kuna tatizo na kuliweka wazi ili liweze kurekebishwa.

  Aidha ameongeza kuwa muswada huo unakusudia kuanzisha Bodi ya Ithibati ya wanahabari ambayo itasaidia katika kuwatambua waandishi wasio wanahabari ambao wanachafua taaalum ya habari.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: UWEPO WA BARAZA HURU LA HABARI UTASAIDIA KUKUZA MAADILI KWA WANAHABARI. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top