728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Sunday, October 30, 2016

  Upendo watajwa kuwa njia mbadala ya kuwarejesha watu wenye makosa katika hali ya kutokuwa waovu.


  Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kuchapisha Magazeti ya Global (Global Publisher Ltd) Bw. Erick James Shigongo(kushoto) akimsikiliza mmoja wa wanakamati ya maandalizi ya Kongamano la Kimataifa la Uongozi(GLS) Bi. Eva Klerruu leo Jijini Dar es Salaam.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kuchapisha Magazeti ya Global Bw. Erick James Shigongo akifanya usajili katika Kongamano la Kimataifa la Uongozi(GLS) leo Jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mkuu wa Uendeshaji wa Kongamano la Kimataifa la Uongozi( Global Leadership Summit) Bw. Peter Mayunga.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kuchapisha Magazeti ya Global Bw. Erick James Shigongo akielezea historia ya maisha yake alipokuwa akiwasilisha maada kuhusu namna ya kurejea katika ndoto ya maisha baada ya kuanguka wakati wa Kongamano la Kimataifa la Uongozi(GLS) leo Jijini Dar es Salaam.Aliyesimama ni Bw. Severin Faustine (55) Aaliyekuwa amefungwa kwa sasa anasaidiwa na Shigongo kwa dhana ya kuwa na upendo kwa wakosaji na si kuwachukia.
  Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Kimataifa la Uongozi( Global Leadership Summit) wakifuatilia mada kutoka kwa wawasilishaji mbalimbali. Kongamano hilo limefanyika na kuwakutanisha viongozi wa Dini, wafanyabiashara na wanasiasa.

  Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Kimataifa la Uongozi( Global Leadership Summit) wakifuatilia mada kutoka kwa wawasilishaji mbalimbali. Kongamano hilo limefanyika na kuwakutanisha viongozi wa Dini, wafanyabiashara na wanasiasa.
  Mwakilishi Mkazi wa Global Leadership Summit nchini Tanzania Bw. Mbutho Chibwaye(kushoto) akimpongeza mshiriki kutoka Kigoma Bi. Gloria Dominicus Kasilo ambaye aliamu kuacha kazi yake ili aweze kushiriki Kongamano la Kimataifa la Uongozi.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kuchapisha Magazeti ya Global Bw. Erick James Shigongo akibadilishana mawasiliano na mshiriki wa Kongamano la Kimataifa la Uongozi(GLS) Bi. Gloria Dominicus Kasilo leo Jijini Dar es Salaam. Mshiriki huyo alikuwa anafanya kazi katika Shirika la Plan International kwenye Kambi ya Wakimbizi ya Nduta lakini aliamua kujiuzulu kazi yake ili aweze kuhudhuria kongamano hilo.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kuchapisha Magazeti ya Global Bw. Erick James Shigongo(wa pili kulia)akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanakamati ya maandalizi ya Kongamano la Kimataifa la Uongozi(GLS) leo Jijini Dar es Salaam.

  Na: Mpiga picha wetu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Upendo watajwa kuwa njia mbadala ya kuwarejesha watu wenye makosa katika hali ya kutokuwa waovu. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top