Mwashungi
Tahir na Fatma Makame/Maelezo Zanzibar
Waziri
wan
chi ofisi ya makamo wa pili ya rais Mohammed Aboud Mohammed amesema
uchumi wa Zanzibar unazidi kuimarika kwa karibu ya asilimia
saba na mfumuko
wa bei bado upo kwenye tarakimu moja na pato la Taifa linazidi kukua.
Ametoa
maelezo hayo ofisini kwake Vuga wakati alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa ilani ya chama
cha mapinduzi Serikali ya awamu ya saba kipindi cha pili cha uongozi wa
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali
Mohammed Shein.
Amesema
katika awamu hii kwa ujumla harakati za uchumi zinaendelea vizuri na ishara
zote za kuimarisha uchumi katika mwaka huu wa fedha zinatoa sura nzuri za
mafanikio.
Akizungumzia
suala la Muungano amesema unaendelea
kuimarika na vikao mbali mbali vya watendaji wakuu wa pande mbili
wakiwemo mawaziri vimeshafanyika na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano ameshafanya vikao viwili vya kisekta kwa nia ya kutatua
changamoto zilizopo.
Waziri Aboud ameelezea kwamba Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar imekamilisha kazi ya kuipandisha hadhi iliyokuwa Idara ya upigaji
chapa na mpigaji chapa mkuu wa serikali na kuwa wakala wa serikali wa uchapaji.
Aidha
amesema kazi ya kufunga mitambo mipya ya uchapaji imekamilika na mafundi wa kiwanda hicho wanaendelea kupatiwa mafunzo ili
kuimudu teknolojia mpya ya mitambo hiyo ili kuongeza ufanisi na
kuongeza upatikanaji wa huduma bora na kwa wakati.
Sambamba na
hayo Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais kupitia Tume ya kitaifa ya kuratibu na
udhibiti madawa ya kulevya imepania kutoa athari za madawa ya kulevya kwa
jamii.
Hivyo Tume
hiyo imefanya kikao maalum na maofisa na wapelelezi wa Jeshi la Polisi wa Mikoa na Wilaya za Unguja kilichoongozwa na mkuu
wa Mkoa Mjini Maghribi kuweka mikakati dhidi ya uingizaji na usambazaji wa
madawa ya kulevya .
Mh
Aboud
amesema ofisi yake inashirikiana na Ofisi ya ukaguzi na mdhibiti mkuu wa
Serikali kuendesha zoezi la uhakiki wa wafanyakazi wa Ofisi ya Makamo
ya Pili
ya Rais na Taasisi zake ili kubaini wafanyakazi hewa.
“Katika
zoezi hili imebainika kwamba Ofisi yetu hakuna wafanyakazi hewa kama inavyobainika sehemu nyengine" alisema
wazirihuyo.
Aidha amesema Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais bado itaendelea kufanya kazi kwa bidii , ufanisi na
tija ili iweze kutoa huduma bora kwa wananchi.
Amesisitiza
kuwa mambo muhimu ya kuzingatiwa hivi sa kwa nchi yetu ni kuimarisha
uzalendo na kusimamia matumizi bora ya ardhi kwani watukishirikiano
katika masulala hayo tutaweza kudumisha amani na upendo na kupiga hatua
zaidi ya maendeleo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed akitoa
tarifa ya mafanikio ya Ofisi yake kuhusiana na utekelezaji wa ilani ya chama
cha Mapinduzi kwa kipindi cha pili cha uongozi wa Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein Ofisini kwake Vuga
Mjini Zanzibar.
Wandishi wa habari wakifuatilia tarifa ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed alipokuwa na mazungumzo nao Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed alipokuwa
akijibu maswali ya wandishi wa habari katika Mkutano wake Ofisini kwake Vuga.Picha na
Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment