728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, October 13, 2016

  TRA WAVUKA MALENGO YA UKUSANYAJI MAPATO ARUSHA

  Meneja wa Mamlaka ya mapato (TRA) mkoani Arusha, bwana Apili Mbaruku.


  Mamalaka ya mapato mkoa wa Arusha (TRA) imekusanya shilingi bilioni 64.6, ikiwa imevuka malengo yake iliyojiwekea awali ya kuweza kukusanya shilingi bilioni 63.1. Ongezeko hilo, ni sawa na asilimia 102, kulingana na meneja wa Mamlaka ya mapato (TRA) mkoani Arusha, bwana Apili Mbaruku. 

  Akizungumza katika mahojiano maalumu na mwandishi wa Globu ya Jamiii mapema leo,Meneja wa mamlaka hiyo mkoa wa Arusha Apili Mbaruku alielezea kuwa ongezeko hilo linatokana na majumuisho ya makusanyo ya mwezi Julai na Agosti mwaka huu. 

  “Ni kweli tumeweza kukusanya kiasi hiki cha fedha, na hii inatokana na
  kukua kwa mwamko wa ulipaji kodi mkoani hapa japokuwa bado zipo
  changamoto kadhaa za baadhi ya wafanyabisahara kutokuelewa umuhimu wa kulipa kodi,” alisema meneja huyo. 

  Apili ametaja sekta ya utalii kuongoza katika ulipaji huo wa kodi. 
  “Tumekuwa tukitoa elimu kwa wafanyabiashara waweze kuelewa umuhimu wa kulipa kodi na kukwepa usumbufu usio na lazima,” alishauri meneja
  huyo. 

  Hata hivyo, Mbaruku aliweka wazi kuwa ofisi yake ilishindwa kufikia
  malengo ya ukusanyi wa mapato kwa mwaka wa fedha 2015/16. 
  “Kwa mwaka uliopita malengo yetu yalikuwa kukusanya shilingi 329.5
  lakini kwa bahati mbaya tulipata shilingi bilioni 324.6 tu”. 
  Na Woinde Shizza,Arusha.

  Akifanunua zaidi kuhusu makusanyo ya mwaka huu, Mbaruku alisema kuwa
  kiasi cha bilioni 30.3 zilitokana na makusanyo ya ndani wakati
  shilingi bilioni sita zilitokana na malipo ya ushuru. Aidha, Mbaruku ameongeza kuwa ofisi yake inatarajia kukutana na
  maofisa wa jiji la Arusha kuanza kukusanya makusanyo ya kodi za
  majengo. 

  Kulingana na meneja huyo wa TRA, ofisi yake inalenga kukusanya kodi
  kutoka kwenye majengo 20, 536 mkoani hapa. Mamlaka ya mapato mkoni
  Arusha(TRA) imevuka lengo la makusanyo yake kwa mwaka wa fedha
  2016/17. 

  “Nia yetu ni kuanza kukusanya kodi kutoka kwenye majengo hayo, na
  tayari tumeshafanya mawasiliano na maofisa wa jiji na kuweza
  kubainisha majengo hayo,” aliongeza meneja huyo wa TRA mkoani Arusha.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: TRA WAVUKA MALENGO YA UKUSANYAJI MAPATO ARUSHA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top